DIWANI MWAMNYANYI AWATAKA WAZAZI KULEA WATOTO KWENYE MAADILI.
DIWANI wa Kata ya Bigwa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Melchior Mwamnyanyi, amewataka wazazi na walezi Kata ya Bigwa kuwalea watoto wao katika maadili mazuri yenye kulinda mila na desturi ili kuendeleza utamaduni wa kitanzania.
Kauli hiyo ameitoa Mei 16/2023 katika maadhimisho ya Siku ya familia duniani yaliyofanyika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo.
Mhe. Mwamnyanyi, amesema wazazi na walezi wanawajibu mkubwa wa kuwafundishwa watoto wao maadili yanayofuata misingi ya Nchi ili kuthibiti wimbi la mmomonyoko wa maadili katika kizazi hiki.
Aidha, amesema kuwekeza kwenye uhifadhi tamaduni, mila na desturi za asili inasaidia kuimarisha utulivu na amani ya Nchi ikiwa ni pamoja na kuzuia migogoro mbalimbali kwenye jamii.
"Niwaombe sana wazazi tuwekeze kwenye malezi na makuzi ya mtoto yanayohifadhi utamaduni wa asili ili kulinda mila na desturi za kitanzania, kufanya hivyo itasaidia watoto kukua katika maadili mema yanayozingatia utamaduni, mila na desturi za makabila yao katika mavazi, heshima na mambo mengine muhimu, na katika vikao wenyeviti ukatili wa kijisnia iwe agenda yenu "Amesema Mhe. Mwamnyanyi.
Pia Mhe. Mwamnyanyi, amesisitizia wazazi na walezi kuwalea watoto katika misingi ya kidini kwa kuhakikisha watoto wanakua katika maadili mazuri yanayozingatia utaratibu wa Nchi ili kutengeneza Taifa bora.
Naye Mtendaji wa Kata ya Bigwa, Helena Mgala, amewataka wazazi kushiriki kikamilifu katika kuhakaikisha watoto wanapata malezi bora.
Naye Chediel Senzighe kutoka Kituo cha msaada wa kisheria (Morogoro paralegal Centre), amesema zipo sheria ambazo zinawaweka hatiani watuhumiwa wamasuala ya ukatili wa Kijinsia ambapo amewataka wazazi kutoa taarifa wanapoona mambo hayo yametokea kwa kuanzia ngazi ya Mitaa hadi Dawati la Polisi ili watuhumiwa kuchukuliwa hatua za kisheria.
kwa upande wa Wazazi , wametumia nafasi hiyo kuishauri serikali kusimamia sheria na sera zinazomhusu mtoto ili kuhakikisha hazileti athari katika makuzi yake.
Wazazi hao, wamepongeza juhudi mbalimbali za serikali zinazofanywa kimkoa na kitaifa kuanza uwekezaji wa makumbusho yanayohifadhi utamaduni wa asili ili kudumisha mila na desturi.
Aidha wazazi hao wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuimarisha utamaduni wa Nchi ikiwa ni pamoja na kutangaza utalii ambapo maeneo mbalimbali ya asili katika jamii yanafikiwa.

Post a Comment