DIWANI MSUYA ATOA UJUMBE KWA WANAFUNZI WANAOSOMEA TAALUMA YA MAENDELEO YA JAMII.
DIWANI wa Kata ya Mbuyuni, Mhe. Samwel Msuya ,amewataka wanafunzi wanaosomea Maendeleo ya Jamii wajifunze taaluma hiyo katika mtazamo mpana ambao utawasaidia kuwajenga katika nyanja yakutatua changamoto zinazozikabili jamiihusika.
Kauli hiyo ameitoa Mei 19/2023 , wakati wa Ofisi yake ya Kata kwa kwa kushirikiana na Kikundi cha Maendeleo ya Jamii cha Community Development Association (C.D.A) kinachoundwa na wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA wakitoa msaada wa vyakula kwenye Makao ya kulelea wazee Funga Funga ikiwa ni mpango wao wa kuona namna ya kusaidia jamii inayokabiliwa na changamoto mbalimbali.
"Leo tupo hapa fungafunga nadhani kuna kitu mmejifunza, hivyo kama wana taaluma ni wajibu kuona umuhimu wa kujali jamii hasa zile zinazoishi katika mazingira magumu. nimpongeze sana Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuona haja kubwa ya kuweka makao ya kulelea wazee na wazee wanapata malezi mazuri " Amesema Mhe. Msuya.
Msuya, amesema wanafunzi hao wanajifunza masuala ya kuutumikia umma lakini lazima wajikite kuangalia uhalisia halisi katika jamii zinazo wazunguka kwani kufanya hivyo wanaweza kuzifikia malengo yakuzisaidia jamii zilizo katika maisha duni.
Kwa upande wa Mtendaji Kata ya Mbuyuni, Sada Mpina, ameishukuru Kikundi cha C.D.A kwa kujitoa kwao na kushirikiana na Ofisi yake huku akiwataka wasiishie hapo kwani bado jamii inahitaji msaada kupitia kwao aidha kwa vyakula au kutoa elimu juu ya maendeleo ya Jamii katika ustawi wa wananchi.
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Mbuyuni,Alicia Mbaga, amewashukuru wanafunzi hao na kuwataka kujifunza kwa vitendo zaidi katika kusaidia jamii kama walivyofanya kupitia michango yao ya kujitolea vyakula.
Mwenyekiti wa C.D.A, Jamaica Magali, amesema Kikundi chao kitaendelea kutoa misaada kadri watakavyoweza kujaaliwa na kuhakikisha taaluma wanayoipata Chuoni wanaitumia kwa manufaa ya jamii inayowazunguka.
Mwakilishi wa Wazee Funga Funga, Mzee Hossea Daniel, ameushukuru Uongozi wa Kata pamoja na wanafunzi wa kikundi cha C.D.A huku akiwataka kuwa makini kwa kuzingatia masomo ili waweze kupata manufaa kwenye maisha yao .
Post a Comment