Header Ads

MBIO ZA MWENGE WA UHURU KUMULIKA MIRADI YA MAENDELEO 68 YENYE THAMANI YA ZAIDI YA TSH.BIL. 12.1.MKOANI MOROGORO.


MWENGE  wa Uhuru 2023 ambao upo chini ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 Bw. Abdallah Shaib Kaim unatarajiwa kuanza kukimbizwa Mkoani Morogoro kuanzia Mei 6 hadi 14 mwaka huu 2023 ambapo unatarajiwa kupitia miradi ya maendeleo 68 yenye thamani ya zaidi ya Tsh Bil. 12.1.

Mwenge wa Uhuru ambao unatoka kukimbizwa Mkoani Iringa utapokelewa Mkoani humo katika Kata ya Chita na kukimbizwa katika Halmashauri zote 9 za Mkoa wa Morogoro na utakabidhiwa Mkoa wa Pwani hapo Mei 15 mwaka huu.


Taarifa iliyotolewa inaeleza kuwa Mwenge wa Uhuru utapitia jumla ya miradi 68 yenye thamani ya Shilingi 12,170,922,197.46 kwa ajili ya Ufunguzi, Uzinduzi, uwekaji mawe ya msingi na kukagua.

Aidha, miradi 24 itawekewa jiwe la msingi, 5 itafunguliwa, 19 itazinduliwa na miradi 20 itakaguliwa.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa ataongoza mapokezi ya Mwenge huo wa Uhuru katika kata ya Chita ukitokea Mkoani Iringa.


Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 zinaenda sambamba na kaulimbiu isemayo “Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai na Uchumi wa Taifa”.

Hima  hima wanamorogoro tushikamane kuupokea mwenge wa Uhuru popote utakapopita.

Miongoni mwa miradi ambayo itapitiwa na Mwenge wa Uhuru kutoka sekta mbalimbali ikiwemo elimu, maji, Afya na barabara.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.