Header Ads

JAMII YAASWA KUTIMIZA WAJIBU KUKABILIANA NA MMOMOMONYOKO WA MAADILI.

DIWANI wa Kata ya Mafiga Manispaa ya Morogoro, Mchungaji Thomas Butabile,  amesema suala la mmomonyoko wa maadili linasababishwa na baadhi ya wanafamilia na viongozi kutokutimiza wajibu wao katika kuhamasisha malezi bora kwenye jamii.

Hayo ameyasema  Mei 18, 2023, katika  kikao kazi cha wanataaluma wa sheria kilichoandaliwa  wanataaluma wa sheria kutoka kikundi cha Youth Led Movement,cha kujadili njia sahihi za kufanya kwa wanataaluma hao katika kuisaidia jamii hususani kulinda maadili ya Mtanzania kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano  Edema Hotel Msamvu.  

Mhe. Butabile,  amesema iwapo viongozi, wazazi, walezi na watoto watatimiza wajibu kuhusu malezi bora kuanzia ngazi ya falimia suala la mmomonyoko wa maadili katika jamii litakuwa historia.

"Wazazi, watoto, wazee wetu, viongozi wa dini na Serikali, hebu tushirikiane katika hili, kila mmoja wetu asimamie maadili, suala hili ni letu sote tushirikiane kukemea maadili yasiyofaa," Amesema Mhe. Butabile.

Mwisho,amesema yupo tayari kushirikiana na vijana yake na Ofisi za Serikali zipo wazi washuke watapokelewa kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi hususani katika mikutano ya Mitaa.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.