Liverpool , Man City zapigana vikumbo saini ya Werner
Klabu ya Liverpool imeingia katika mbio na Manchester City kuwania saini ya Mshambuliaji wa RB Leipizg ya Ujerumani, Timo Werner.
Kwa mujibu wa jarida la Kijerumani, Bild, limeandika mchezaji huyo anaweza akaachana na Leipzig inayoshika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi hivi sasa baada ya msimu huu kumalizika.
Jarida hilo limeeleza kuwa Klopp anahitaji huduma ya mchezaji huyo ili aweze kuimarisha zaidi safu ya ushambuliaji wa kikosi chake.
Vilevile taarifa zinasema Kocha Klopp ameshaanza mazungumzo na wakala wa mchezaji huyo, Karlheinz Forster, ili kukamilisha mchakato wa kumsajili Werner.
Dau la pauni milioni 87 ndiyo linalotajwa kuweza kumuondoa Werner ndani ya kikosi cha Leipizg, katika msimu wa majira ya joto.

Post a Comment