Header Ads

Diwani Kata Tandika afungua Baraza la Kata Uvccm kwa kishindo

DIWANI wa Kata ya Tandika kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Dkt Ramadhani Likimangiza leo amefungua mkutano wa Baraza la Uvccm kwa mara ya kwanza tangia Jumuiya hiyo ishike nyadhifa ya kuongoza kata hiyo.
Diwani Kata Tandika afungua Baraza la Kata Uvccm kwa kishindo
kizungumza na waandishi wa habari mapema leo kwenye Ofisi ya Kata ya Tandika, Dkt Likimangiza amesema kuwa Vijana ndio jeuri ya Chama pamoja na tanuli la kupikia Viongozi hivyo kama watatumia vyema fursa walizonazo watakifikisha mbali chama na watu wengi kuwajengea imani juu ya utendaji wa CCM.

Diwani Likimmmangiza amesema kuwa siri ya ushindi wa  Chama cha CCM  ni pamoja na kushughulikia matatizo ya Wananchi , hivyo kuna kila sababu ya kujenga umoja na mshikamano ili kulinda misingi ya Chama.

 Amempongeza Rais John Magufuli kwa jitihada za dhati za kukirudisha Chama kwa masikini na wanyonge huku akisema anadhamirra ya dhati ya kumkomboa mtanzania kupitia awamu yake ya tano.

Aidha, Diwani Likimangiza amekili uwepo wa fedha zilizoingia kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kwa ajili ya kuwakopesha wananchi kwani asilimia 10 iliyotengwa kupitia makusanyo ya kila Manispaa ya kila baada ya miezi mitatu ni pesa ya wananchi hivyo lazima warudishiwe pesa zao kwa ajili ya maendeleo mengine.

Ameeleza wazi kwamba katika fedha iliyoingia katika Manispaa ya Temeke katika awamu ya kwanza ni sawa na shilingi milioni 17 na laki tano lakini kiasi hicho kiliongezeka hadi kufikia shilingi milioni 36 laki saba na elfu hamsini lakini nyongeza hiyo itaongezeka hadii kufikia shilingi milioni 43.

''Natakuwaeleza Vijana wangu, changamkieni fursa, pesa iliyotolewa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ni mali ya wananchi wote ni pesa yetu ya kodi hivyo nawaagiza kila kikundi kijisajiri na majina niyapate niyapeleke kwa afisa maendeleo wa kata ili ayaingize katika mgawanyo wa mikopo'"amesema Likimangiza
  
Miongoni mwa pesa ambazo zitagawiwa katika mgao huo zimetengwa katika vikundi 24 ambapo kila kikundi kina jumla ya watu 74, ambapo jumla ya watu 23 ni wanawake na watu 51 Vijana.

Hata hivyo amesema atahakikisha anapambana katika vikao vya baraza na kupelekea malalamiko yake DCB ili asilimia 4 ya wakina mama ipitie moja kwa moja katika Majukwaa ya kina Mama japo haitakuwa kazi rahisi lakini ameomba wakinamama wote wamuunge mkono.

Katika hatua nyingine, Katibu wa Kata ya Tandika, Salumu Machado..amesema ni wakati sasa Jumuiya kujenga watu watakao stahili kugombea 'nafasi ya wenyekiti wa mtaa unaotarajiwa kufanyika mwakani 2019.

Amewataka  Uvccm kujenga umoja thabiti utakaowafanya kutetea viti vyao vilivyochukuliwa na wapinzani ili CCM izidi kushika dola katika kuwatumikia wananchi na kuleta maendeleo kijani huku akisema Ofisi yake ipo wazi kushughulikia changamoto za Vijana.

Hata hivyo, Mwneyekiti wa Uvccm Kata ya Tandika, Salehe Malegula, amewataka wana CCM kata ya Tandika kuwa nasubira wakati wakianza upya kusuka Uvccm.
Mwenyekiti wa Uvccm Kata ya Tandika, Salehe Malegula akizungumza jambo mbele ya wajumbe wa baraza la Kata leo
  "Huu ndio mwanzo, tangia tuingie madarakani hatujawahi kufanya kikao cha baraza la kata hata siku moja kutokana na changamoto, sasa tunaanza kujenga upya Jumuiya yetu, wale amabao watahitaji kuungana nasi wazidishe utendaji wa kazi na wale ambao watakuwa kinyume na sisi tutawashughulikia hatuhitaji viongozi majina tunataka watu wa kazi katika kuifanya CCM mpya"amesema Malegula 
Katibu wa Uvccm Kata ya Tandika 
Katika hatua nyingine, Uvccm Kata ya Tandika inakabiliwa na ugeni mkubwa kutoka Wilayani mnamo tarehe 15 mwezi Aprili, 2018 lengo likiwa kukagua maendeleo ya Jumuiya na kuona changamoto zianzowakabaili na kuzichukulia ufumbuzi.


JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.chombohuru.blogspot.com ku-install App ya chombo huru bila ya kuingia websiteTweet@chombo Huru online, youtube@Chombo hurua online TV, Fb@Chombo huru online, insta@chombo huru online

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.