Header Ads

Mfaransa wa Simba acharuka mazoezini

Kocha Mkuu wa Simba, Pierre Lechantre, juzi Jumatano, alijikuta akiwa mwenye hasira katika mazoezi ya timu hiyo, yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Boko Veterani, na kuwafokea vikali wachezaji waliokuwa wakifanya utani na kuharibu ratiba yake ya mazoezi.
Image result for Kocha Mkuu wa Simba, Pierre Lechantre
Pierre ambaye ni raia wa Ufaransa ana zaidi ya miezi miwili tangu aanze kuionoa Simba, baada ya kuchukua kijiti hicho kutoka kwa Mcameroon Joseph Omog, pia alikuwa mbogo hata kwa msaidizi wake, Masoud Djuma.

Mfaransa huyo alimlaumu Djuma kwa kutochukua hatua baada ya wachezaji kufika mazoezini na kutoanza ratiba wakati anafahamu kila kitu kuhusiana na muda ambao wamejipangia kuanza mazoezi yao.

Alipomalizana na Djuma, kocha huyo alimuita kiungo mkongwe Mwinyi Kazimoto na kuanza kumwambia juu ya kuvurugwa kwa ratiba hiyo, alipomalizana nao akawakusanya wachezaji pamoja na Djuma na kuanza ‘kuwakoromea’ kwa pamoja.

Baada ya muda akamuachia Djuma aendelee kuwaelekeza kisha akamfuata meneja wa timu hiyo, Richard Mutui akazungumza naye kwa dakika kadhaa na kurejea katika majukumu yake ya kufundisha.

Sehemu ya kauli ambazo alitamka kocha huyo kwa wachezaji ni kusema: “Hivi inakuwaje ratiba na program nzima ya mazoezi mnaifahamu lakini mmeshindwa kuanza, nimewafuatilia tangu saa 10:00 na sasa ni zaidi ya robo saa imepita hamuonyeshi hata hali ya kuanza mnamaanisha nini!

“Uzembe huu siwezi kuuvumilia hata kidogo na wala nisingependa kuwaona mkirudia haya siku nyingine.”

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.