Header Ads

Kampuni mbili zachunguzwa Uganda kwa kusambaza dawa feki

Dawa feki zilikutwa kwenye vituo vya afya vya binafsi
Image captionDawa feki zilikutwa kwenye vituo vya afya vya binafsi
Kampuni mbili nchini Uganda zinachunguzwa baada ya kuhusishwa na kitendo cha kusambaza dawa feki za chanjo ya homa ya ini kwa vituo vya afya vya binafsi.
Wizara ya Afya nchini humo imenukuliwa na Gazeti la serikali la New Vision ikisema kuwa kuna uwezekano kuwa chanjo ni halisi lakini lebo zake zimebadilishwa.
Kwa mujibu wa mamlaka ya taifa ya dawa ya Uganda, inayofanya uchunguzi sambamba na wizara ya afya, dawa hizo zilikutwa kwenye hospitali nane na zahanati jijini Kampala, na miji mingine kama vile Mbale,Entebbe na Mbarara.
Moja ya zahati hizo imekana kutumia ''chanjo feki''
''Huduma zetu ni za ngazi za kimataifa...dawa zote zinazotumika kwenye hospitali zetu zinafanyiwa majaribio kwa ajili ya kuangalia ubora wake'', alieleza msemaji wa kituo cha afya cha Univic Medical kilichopo Kampala akinukuliwa na gazeti linalomilikiwa na kampuni binafsi, Daily Monitor.
Lakini mamlaka ya dawa inasema iliziona dawa zinazodaiwa kuwa feki kwenye kituo hicho cha afya.
Daily Monitor limeripoti kuwa Mtandao wa kupambana na bidhaa feki Afrika umeitaka serikali ya Uganda kueleza chanzo cha chanjo ya homa ya ini kuingia nchini humo na namna gani ziliingizwa.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.