moja atumbuliwa ziara ya CCM Wilaya ya Ilala, Chuma ataka Chama kiheshimiwe
Mwenyekiti CCM Wilaya ya Ilala Ubaya Chuma amemtumbua mjumbe wa ccm shina namba 14 tawi la sabasaba kata ya Ukonga kwa kutokubaliwa na wanachama pamoja na wananchi walio wengi kutokana na kuwa na utendaji mbovu wa kazi , kauli mbaya kwa wanachama wenzake pamoja na kuweka mbele maslahi yake binafsi.
Hayo ameyafanya katika muendelezo wa ziara yao ambapo pia amewataka viongozi wote wa mashina wanaojilimbikizia vyeo, kupunguza vyeo hivyo ili kuwapa nafasi na wengine..
Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti Ubaya Chuma amesema kuwa lengo la ziara hiyo ni kushuka katika matawi pamoja na mashina yake ili kuweza kutathimini uhai wa chama.
Amesema kuwa utaratibu huo wa kutembelea mashina ulikufa miaka 30 iliyopita, huku kwa sasa ukirudishwa tena na Mwenyekiti CCM taifa, ambaye pia ni Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
"Na CCM ngazi ya Wilaya kumekaa na tumeamua kufuatilia kuona na kuthibitisha uhai wa chama na kuona kama viongozi hawa walichaguliwa kihalali.
Aidha amewataka viongozi wa mashina kuwa na utaratibu wa kufanya vikao kila mwezi ili kuweza kujadili changamoto zinazowakabili na kuziandikia muktasari ili kuzifikisha ngazi usika na kutafutiwa ufumbuzi.
Kwa upande mwingine wanachama wa CCM Wilaya ya Ilala wameombwa kuendelea kumuombea mwenyekiti wao na Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Katika juhudi zake za kuwatumikia wananchi licha ya baadhi ya watu kubeza utendaji kazi wake.
Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na katibu wa CCM Wilaya ya Ilala Joyce Ibrahim wakati wa ziara amesema kuwa wanahitaji viongozi ambao wanawatumikia wananchi na watahakikisha kuwa heshima ya chama inarudishwa kwa wanachama na sio viongozi kwani wote wanahaki sawa ndani ya chama chao.
Kwa upande wake Mjumbe wa halmashauri kuu ya mkoa Mashaka Nyadhi amewataka viongozi wa mashina kuhakikisha wanasimamia utaratibu wa uendeshaji wa chama ikiwemo idadi ya wanachama ndani ya shina, uchaguzi uendeshwe kwa mujibu wa katiba.
Ziara hiyo ambayo ilianza Machi 9 -26 mwaka huu imetembelea kata 26 na ndani ya Jimbo la ukonga na segerea nakubakiza kata 10 ambazo zitamaliziwa mwisho wa mwezi huu na kufanikiwa kutembelea mashina zaidi ya elfu mbili pamoja na wanachama 78 eflu ambapo ziara hiyo imefanikiwa kwa asilim
Post a Comment