Diwani Kijichi awashukia waalimu wanaochangisha michango shuleni
DIWANI wa Kata ya Kijichi kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM , Elias Mtarawanje, amesema anakerwa sana na waalimu wanaokiuka maagizo ya Rais John Magufuli ya elimu bure huku baadhi yao wakionekana kushindwa kuendana na utendaji wake.
Akizungumza leo mapema na Waandishi wa habari, katika Shule ya Msingi Mtoni Kijichi iliyoko Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam, Mtarawanje, amesema ifike wakati Waalimu waheshimu maagizo ya Rais kwani kwenda kinyume na maagizo hayo ni dalili za dharau na ukiukwaji wa sheria.
Mtarawanje amesema kuwa, endapo atawabaini waalimu wanaojihusisha na kula pesa za wanafunzi kwa kuwachangisha wazazi atadili nao na kamwe hatakuwa na msamaha.
Amesema anafahamu fikra kwamba changamoto za waalimu ni kubwa hivyo madai wanayodai pamoja na stahiki zao haziwezi kukidhi mahitaji yao kulingana na kazi wanyoifanya huku wakitumia muda mwingi sana kukaa shuleni bila ya kuwa na vitega uchumi vya kuwaingizaia pesa.
"Niwaombe Waalimu wangu au wataaluma wangu, zingatieni sana maadili ya kazi zenu, fanyeni kazi kwa bidii watumikieni wanafunzi wenu kwa ufasaha, haya mambo ya kuchangisha wanafunzi yashapigiwa marufuku, sitarajii kuona mwalimu au bodi ya shule wakidiriki kuchangisha michango, kwani Rais John Magufuli alishatoa tamko na hakuna wakilivunja, wale watakao kiuka maagizo haya nitawashughulikia mara moja, nitaanza na waalimu, Wenyeviti wa bodi pamoja na Afisa Elimu wa Kata"amesema Mtarawanje
Aidha , Mtarawanje amewataka waalimu pamoja na bodi zao kama wanataka Ofisi za Waalimu zikamilike mapema lazima wafuate maagizo kutoka Ofisi ya Mkoa wa Dar Es Saalaam iliopo chini ya RC Makonda, kuwa na kokoto, mawe na mchanga ndipo watasaidiwa kwa urahisi na Ofisi hizo zitajengwa kisasa.
Pia amesema ili kuboresha miundombinu ya Waalimu Shuleni ni lazima kila shule ihakikishe inazingatia maagizo hayo na yeye akiwa diwani atajitolea kila shule malori ya michanga mawili ili kufikia ujenzi huo ambao utaleta tija.
Katika hatua nyingine, Mtarawanje, amesema yupo mbioni kuanzisha mashindano ya wanafunzi watakao fanya vizuri na kuwapa zawadi lengo likiwa ni kuongeza hari ya utendaji ili kufikia matokeo makubwa.
Vile vile amesema kuwa, atahakikisha waalimu wanafanya safari za kutoka nje ili kubadili mazingira kila mwisho wa mwaka lengo likiwa ni kubadilisha fikra na akili kwa waalimu baada ya kukabiliwa na kibarua kizito cha kufundisha na kuleta matokeo chanya yatakayo letea maendeleo Taifa letu.
Lakini hakuwaacha mbali walimu baada ya kusema nawao watakuwa na "Diwani award" ili kuamsha hai ya kiutendaji baina ya waalimu katika kufanikisha matokeo makubwa yanapatikana na zawadi zitakuwa kubwa na kumbukumbu katika maisha ya walimu.
Hata hivyo, amewataka waalimu kupunguza adhabu za viboko vikali kwa baadhi Wanafunzi wa kike, kwani kesi nyingi zimekuwa zikipelekwa katika Ofisi yake huku baadhi ya wazazi wakilalamika adhabu kali na kuwaweka watoto zao katika hali isiyo ya kiusalama hususani watoto wa kike ambao wana magonjwa yao.
Katika kuhitisha hayo, amewataka waalimu wote wazidi kushirikiana nae kwa kila jambo kwani yeye ndiye mwenyekiti wa kamati ya maendeleo hivyo amewaomba pia washirikiane vyema na wananchi wake kwani wasipofanya hivyo hata yeye atakuwa mzito kushirikiana na waalimu hao kufikia mafanikio na malengo waliyojiwekea.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.chombohuru.blogspot.com ku-install App ya chombo huru bila ya kuingia websiteTweet@chombo Huru online, youtube@Chombo hurua online TV, Fb@Chombo huru online, insta@chombo huru online

Post a Comment