Abdulrahman kuanza dhidi ya Congo
Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Hemed Morocco, amesema maandalizi ya mchezo wa kesho dhidi ya Congo yameenda vizuri lakini mechi haitakuwa mrahisi.
Morocco ameyasema hayo ikiwa imesalia siku moja ambayo ni leo kuelekea mchezo huo wa kirafiki wa kalenda ya FIFA utakaopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kuelekea mchezo huo, Morocco amesema Stars itawakosa wachezaji, Abdulazizi Makame ambaye aliumia mazoezini pamoja na Mlinda Mlango Aishi Manula ambaye bado hajapona majeraha yake.
Kukosekana kwa Manula kutamfanya Golikipa aliyeanza dhidi ya Algeria, Mohammed Abdulrahma kuanza dhidi ya Congo pia.
"Tutawakosa Aishi Manula ambaye bado hajawa fiti, hivyo kipa aliyeanza dhidi ya Algeria ataendelea kuwa langoni, vilevile Makame naye hatoweza kucheza baada ya kuumia mazoezini" amesema Morocco.
Mbali na hayo, Morocco amesema wanahitaji kushinda mechi hiyo ili wajiweke pazuri katika viwango vya ubora wa soka duniani (FIFA).

Post a Comment