Header Ads

Meya Chaurembo azindua Jukwaa la Wanawake Mtaa wa Sigara Yombo Vituka

MEYA wa Temeke Abdallah Chaurembo, amefungua Jukwaa la Wanawake la Mtaa wa Sigara lililopo Kata ya Yombo Vituka Wilaya ya Temeke.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo mapema Jijini Dar es Salaam Sigara Yombo Vituka wakati wa uzinduzi huo, amesema ni wakati sasa wa Wanawake kutumia fursa ambayo Makamu wa Rais Samia Suluhu aliyowapatia wakina mama ili kujikwamua kiuchumi na kuondokana na maisha tegemezi.
Meya Chaulembo amewataka Wanawake hao kama wanahitaji kufikia malengo yao basi waachane na matumizi yasiyo ya lazima ambayo yanakwamisha uchumi wao na kutofikia malengo.

Katika upande wa mikopo, Meya Chaurembo amesema kuwa, suala la kupanda kwa riba kubwa katika benki kunatokana na baadhi ya Kata katika Halimashauri ya Manispaa ya Temeke kushindwa kurejesha mikopo hiyo ipasavyo, miongoni mwa kata ambao zilishindwa kulipa madeni ni pamoja na Kata ya Kata ya Tandika, Sandali pamoja na Kijichi ambazo  hazija fanya vizuri katika marejesho ya mikopo ya fedha.
Hata hivyo, amesema asilimia 10 ambazo zinatolewa na Halimashauri ya Manispaa ni kiasi kidogo sana cha pesa ambacho wakina mama wanatakiwa kupewa lakini amesema wizara ya afya kwa kushirikiana na wiara ya kazi wanawajibu wakutenga fedha ili kufikia malengo ya mikopo inayotolewa.
Hata hivyo amefafanua kwamba baada ya kushindwa kurejesha mikopo kwa ufanisi, pesa hizo waliamua kuzielekea DCB lakini kutokana na Benki hiyo kuwa na mikopo mikubwa ambayo sio rafiki kwa kumkomboa mwanamke na badala yake wanatumia nafasi ya kumkandamiza.
Mtendaji wa Mtaa wa Sigara akivishwa taji na Meya Chaurembo wakati wa kusikmika Viongozi wa Jukwaa la Wanawake
Amesema kuwa ametangaza tenda kwa Benki ambazo  zitakuwa na riba ndogo zitakazo kizi mahitaji ya kumkomboa mwanamke ndizo watakazo zitumia, miongoni mwa Benki ambazo mpaka sasa amezipendekeza ni pamoja na Equity Benki.
Diwani wa Kata ya Yombo,Kpateni Dicken Makinda (kushoto) akizunguma jambo na Jukwaa la wanawake la Mtaa wa Sigara  mara baada ya kupata nafasi ya kumkaribisha Meya Chaurembo
“Nawashauri wakina mama kama mnahitaji kukopa basi mkakope kulingana na na biashara yako na sio kukopa kiwango kikubwa cha fedha ambacho hakilingani na biashara unayoifanya , kwa kufanya hivyo mtaweza kurejesha mikopo yenu kirahisi na kuondokana na usumbufu kutoka benki”amesema Chaurembo .
Vile vile amesema kwamba baadhi ya wakina mama wengi wanashindwa kutofautisha biashara na matumizi ya nyumbani, hivyo mewataka kama wanahitaji elimu ya kibenki ni lazima wajifunze kuwekeza kidogo kidogo
Amesema ameshaongea  na DCB kuhakikisha kila Kata ya Temeke inapatiwa  milioni 43 na hizo fedha zitaelekewa kwenye Majukwaa hivyo wale wasio na Majukwaa wajiunge na wajisajili ili wanufaike na mikopo hiyo
Hata hivyo amelitaka Jukwaa Wanawake la Sigara kusajili huku yeye akiahidi kushirikiana nao bega kwa bega ili kuwea kupata mikopo ya Halimashauri na kuchangia shilingi laki saba katika kutunisha mfuko huo.  


Katika hatua nyingine, amewahakikishia kuboresha miundombinu ya bara bara pamoja na kupanua huduma ya afya katika Zahanati ya Sigara na kufanya huduma zote kama ilivyo Zahanati ya Kata ya Yombo, kwani mpango walionao sasa ni kuona Zahanati ya Yombo ya Kata inakuwa na hadhi ya kituo cha afya huku huduma ambazo zilikuwa ikitolewa na Hospitali ya Temeke zitolewe Kata ya Yombo hivyo katika kufanikisha hilo wametenge Bilioni 2.7 kujenga kituo hicho cha afya chenye Gorofa tatu.
Naye Mwenyekiti wa Jukwa la Wanawake Mtaa wa Sigara, Emmy Sanga, amesema lengo lao ni kuhakikisha huduma za mikopo zinawafakia wakina mama wote na wananwake lakini akasisitiza ili uweze kupata mikopo kwa pamoja ni lazima ujiunge na Majukwaa haya.

Amempongeza Makamu wa Rais Samia Suluhu kwa kuwajali wakina mama katika mpango wake wa kuwakomboa kiuchumi ili waondokane na maisha tegemezi kutoka kwa mume zao au jamii inayowazunguka.

  
Katibu wa Jukwaa hilo, Modesta Boniface amesema changamoto zipo nyingi kama vile ukosefu wa elimu ya ujasiriamali, soko, miundombinu sio rafiki kwa magari kufika eneo la soko hivyo akatoa wito wake kwa Serikali na mgeni rasmi kuwasaidia kero hizo ili wafanikishe ndoto zao.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.chombohuru.blogspot.com ku-install App ya chombo huru bila ya kuingia websiteTweet@chombo Huru online, youtube@Chombo hurua online TV, Fb@Chombo huru online, insta@chombo huru online

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.