Mtoto wa miaka 9 amuua nduguye kwa kumpiga risasi Marekani
Mvulana wa miaka tisa nchini Marekani anadaiwa kumuua dadake wa miaka 13 kwa kumpiga risasi kichwani baada ya mzozo kuhusu kifaa cha kudhibiti mchezo wa video wa kompyuta, polisi wanasema.
Mvulana huyo katika jimbo la Mississippi anadaiwa kuchukua bunduki Jumamosi alasiri baada ya dadake kukataa kumpa kifaa hicho.
Alimpiga risasi kichwani kutoka kisogoni, na risasi hiyo ikaingia hadi kwenye ubongo.
Liwali wa eneo hilo alitangaza Jumapili kwamba mvulana huyo alifariki akitibiwa katika hospitali ya Memphis.
Haijabainika ni vipi mvulana huyo alipata bunduki hiyo na pia bado haijabainika ni hatua gani zitachukuliwa dhidi yake.
"Ni mtoto wa miaka tisa tu," liwali wa tarafa ya Monroe Cecil Cantrell aliambia gazeti la Clarion Ledger.
- Bwana harusi apigwa risasi katika sehemu nyeti Misri
- Mtoto azaliwa na risasi mwilini nchini Marekani
- Mwanamume ajipiga risasi na kujiua nje ya White House
"Nafikiria kwamba ametazama hili kwenye michezo ya video ya kompyuta au kwenye runinga. Sijui iwapo alifahamu hasa nini alichokuwa anakifanya. Siwezi kujibu hilo. Najua tu kwamba ni mkasa, kisa cha kusikitisha."
Mama ya watoto hao alikuwa kwenye chumba kingine, akiwalicha watoto wengine kisa hicho kilipotokea.
Polisi wanachunguza kisa hicho, ikiwa ni pamoja na jinsi mtoto huyo aliweza kuifikia bastola hiyo ya risasi za kiwango cha .25.
"Hili ni jambo geni sana kwetu, hatujawahi kukumbana na mtoto wa miaka tisa aliyempiga risasi mtoto mwenzake," liwali Cantrell aliambia vyombo vya habari.
Post a Comment