Trump aonywa asivuruge uchunguzi wa Mueller
Rais Donald Trump ameonywa na wanachama wa chama chake cha Republican kuacha kuingilia uchunguzi maalumu kuhusiana na Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani uliopita.
Hatua hii ya wanachama wa Republican inakuja baada ya rais Trump kumshambulia kuhusiana na uchunguzi wake dhidi ya Urusi kudaiwa kuingilia uchaguzi wa mwaka 2016.
Ktika ukurasa wake wa Twitter mwishoni mwa juma,Trump alirejea kutoa utetezi wake amesisitiza kuwa hakukuwa na uhusiano wowote kati ya timu yake ya kampeni na Urusi na kusema kuwa hiyo ni vita binafsi inayoshabikiwa na Democrats.
- Mkurugenzi wa FBI aliyefutwa kazi 'amwaga mtama' kuhusu mazungumzo na Trump
- Sababu zilizomfanya Trump kumpiga kalamu Rex Tillerson
- Trump amfuta kazi Waziri wa mambo ya nje Tillerson
Mueller,ambaye ni mkuu wa zamani wa FBI, anaungwa mkono na Republican kuendelea na uchunguzi wake bila kuingiliwa.
Senata Lindsey Graham amesema Trump asijaribu kuchukua hatua yoyote dhidi ya Mueller ikiwemo kujaribu kumfuta kazi.
"Akijaribu kufanya hivyo, itakuwa mwanzo wa miwsho wa madaraka yake, sababu sisi ni taifa la kufuata sheria," Bwana Graham alisema.
Post a Comment