Utafiti: Upungufu wa mbegu za kiume unahatarisha maisha
Wanaume wenye mbegu chache za kiume wako katika hatari ya kupata magonjwa kulingana na utafiti mpya.
Utafiti uliofanyiwa wanaume 5.177 ulibaini kwamba wanaume wenye mbegu chache za kiume wana mafuta mengi mwilini , shinikizo la damu na mafuta machafu katika mishipa ya damu.
Pia wana uwezo mkubwa wa viwango vidogo vya homoni za kiume. Waanzilishi wa utafiti huo wamesema kuwa , wanaume wenye mbegu chache za kiume pia ni muhimu kufanyiwa vipimo vyengine vya magonjwa mengine.
Hivi karibuni nchini Tanzania kumeshamiri kwa uwepo wa matangazo mbalimbali ambayo mengine ni rasmi na mengine sio rasmi kuhusiana na dawa za asili haswa za kuongeza nguvu za kiume lakini sasa serikali ya nchi hiyo imethibitisha matumizi ya dawa tano za asili.
- Dawa tano za asili zaidhinishwa Tanzania
- Utafiti: Vipande vya plastiki vyapatikana katika maji ya chupa
- Magufuli awahimiza Watanzania wazaane kwa wingi
Huku miongoni mwa dawa hizo ni dawa ya 'Ujana' ambayo kazi yake ni kusaidia kuongeza nguvu za kiume wakati dawa nyingine zikiwa Sudhi, Vatari, IH Moon na Coloidal Silver ambazo kazi yake ni kukemea vimelea mbalimbali.
Baraza la dawa nchini humo limesema hatua hii imekuja baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na kubaini kuwa dawa hizo hazina madhara kwa afya ya binadamu hivyo hawana budi kuzikubali.
Aidha Paul Muhame ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa dawa za asili nchini Tanzania anasema baada ya baraza kupitisha vigezo vyote vilivyohitajika kutoka katika dawa hizo na mamlaka ya dawa na chakula wamethibitisha hilo.
"Suala la muhimu ambalo tumeliangalia zaidi ni usalama wa mtumiaji lakini katika upande wa kuthibitisha kuwa dawa hizo zinaponyesha au la, linabaki kwa mnunuaji na mtumiaji wa dawa hiyo''.
'Hatari'
Upungufu wa mbegu za kiume na matatizo ya ubora wa mbegu hizo ni maswala yanayoathiri mmoja kati ya wanandoa watatu kushika mimba kulingana na utafiti huo uliofanywa nchini Uingereza.
Lakini katika utafiti huu mpya wanasayansi walichanganua wanandoa wasioweza kupata watoto nchini Itali kujua iwapo ubora wa mbegu hizo pia unaathiri afya ya mtu kwa jumla.
Waligundua kwamba wanaume wengi walio na mbegu chache walikuwa na matatizo kadhaa ya kiafya ikiwemo mwili ulionenepa na shinikizo la damu.
Hatua hiyo huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari, magonjwa ya moyo na kiharusi.
Wanaume hao pia walionekana kuwa na viwango vya juu vya kuwa na homoni chache za kiume ambazo hupunguza ukubwa wa misuli na mifupa na huenda vikasababisha ugonjwa wa kudhoofika kwa mifupa.
Daktari Albert Ferlin ambaye aliongoza utafiti huo , alisema: Wanaume wasio na rutuba hukumbwa na matatizo ya kiafya ambayo yanaweza kuhatarisha hali yao ya maisha na kupunguza kiwango cha maisha wanayoishi. ''Rutuba huwapatia wanaume fursa isio ya kawaida ya kutathmini afya na kuzuia magonjwa''.
Hatahivyo wamiliki wa utafiti huo walisisitiza kuwa utafiti wao haukuthibitisha kuwa ukosefu wa mbegu za kiume za kutosha husababisha matatizo ya kimetaboliki lakini badala yake ni vitu viwili vinavyohusiana.
Wanasema kuwa uhaba wa homini za kiume uhusishwa na matatizo haya ya kiafya.
Dr. Ferlin alisema kuwa utafiti unaonyesha kwamba ni muhimu kwa wanaume wanaotibiwa matatizo ya ukosefu wa rutuba wanafaa kuangaziwa vizuri kimatibabu.
''Wanaume walio na matatizo ya kuwapatia mimba wake zao wanafaa kukaguliwa vizuri na kufuatiliwa na wataalam wao wa rutuba kwa sababu huenda wana viwango vya juu vya kupata maradhi na vifo'', alisema.
Hatahivyo uthibitisho wa dawa za asili nchini Tanzania umezua mjadala mkali katika vipindi vya radio nchini humo haswa katika upande wa serikali kuthibitisha dawa za nguvu za kiume kuuzwa kihalali .
BBC iliweza kupata maoni mbalimbali kutoka kwa Watanzania kuhusiana na uthibitisho wa dawa hizo:
'Watu watazinunua lakini hakuna mtu atakuwa na uhakika kwamba dawa hizi zinatibu sana sana atabahatisha tu,"
" inaweza isilete madhara lakini huwezi kujua baadae lakini kiukweli inabidi ziangaliwe kwa watu maalum kwa watu wanaouza ili mtu akidhurika ajue ataenda kwa nani?" Thomas Hemed ,mkazi wa Dar es salaam amesema
Sababu za kukosa nguvu za kiume:
- Magonjwa (kisukari, saratani)
- Msongo wa mawazo
- Kutumia aina fulani ya dawa kwa mfano dawa za kudhibiti msukumo wa damu (BP)
- Umri mkubwa
- Kukosa usingizi wa kutosha
- Matatizo ya kihomoni
Post a Comment