Header Ads

CHIEF YARED AONGOZA KIKAO CHA SEKRETARIETI CCM TABORA MJINI KAMA SEHEMU YA KUSHEHEREKEA MAPINDUZI MATUKUFU YA ZANZIBAR KWA KUTEMBELEA SOKO KUU NA MACHINGA COMPLEX.





Katibu wa CCM Wilaya ya Tabora Mjini, Chief Sylvester Yared,  ameongozana na  Sekretatieti yake ya Wilaya sambamba na Wataalam wa Afya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Leo tarehe 12 Januari 2024 kama sehemu ya kusheherekea Mapinduzi matukufu ya Zanzibar kwa kutembelea Soko kuu na Machinga complex.         

Chief yaredi amefanya ukaguzi katika maeneo Wafanyabiashara wanahifadhia taka ngumu na ametoa maagizo ya Chama kwa watendaji wa Serikali  ndani ya siku sita tu kuhakikisha unafanyika usafi wa hali ya juu ili kuepukana na magonjwa ya milipuko.

Aidha ili  kuhakikisha eneo la kuhifadhia Taka ngumu linawekewa Changarawe na Kuitaka Manispaa kuanza mchakato wa kujenga vyoo vipya ili kuendana na Hali ya sasa ya Manispaa 

Aidha, Chief Sylvester Yaredi amewataka wananchi kuendelea kumuunga Mkono Mheshimiwa Rais Dr. Samia  Suluhu  Hassan Na  kuendelea kuwa na imani na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM).                                                                   

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.