WAZEE NGAZENGWA WAKARIBISHA MWAKA KWA KUFANYA SHEREHE NA KUTUNISHA MFUKO WA BARAZA
BARAZA la Wazee Mtaa wa Ngazengwa Kata ya Uwanja wa Ndege Manispaa ya Morogoro, wamefanya sherehe ya pamoja ikiwa na lengo la kukaribisha mwaka 2024.
Sherehe hizo zimefanyika kwenye Ukumbi wa Kingalu Soko Kuu la Morogoro Januari 15/2024 na kuhudhuriwa na Viongozi wa Baraza la Wazee la Manispaa na Mratibu wa Wazee Manispaa.
Akizungumza katika hafla hiyo ya kukaribisha mwaka , Katibu wa Baraza la Wazee Manispaa ya Morogoro , Dkt. Bakili Anga, amesema lengo la sherehe hiyo ni Wazee kujumuika pamoja kufurahia katika kukaribisha mwaka mpya 2024.
Kwa upande wa Mratibu wa Wazee Manispaa ya Morogoro, Hamisa Kagambo, amepongeza Uongozi wa Baraza la Wazee Ngazengwa kwa kuanzisha utaratibu huo ambao ukiigwa na Mabaraza mengine utakuwa mzuri kwani unawakutanisha wazee kukaa pamoja na kujua changamoto za pamoja na kuzitatua.
“Shughuli hizi za kukutanisha watu pamoja zinajenga jamii, niombe sana Mabaraza muendeleze huu utamaduni ambao wenzenu wa Ngazengwa wameuanzisha, huu ni utamaduni mzuri hata mkiafanya kwenye maeneo yenu hakuna tatizo lolote linalotokea,niwapongeze sana kwa kuunganisha jamii za wazee ”Amesema Kagambo.
Katika kusherehekea kukaribisha mwaka , mbali na washiriki kula,kupata vinywaji,kucheza pia kuliendeshwa zoezi la kuchangia keki kama sehemu ya kutunisha mfuko wa Baraza la Wazee la Ngazengwa.
Post a Comment