Header Ads

BILIONI 18 ZA RAIS SAMIA KUMALIZA KERO YA MUDA MREFU YA MAJI KIHONDA, LUKOBE NA MKUNDI-RC MALIMA

MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima , amekagua miradi  ya maji miradi inayotekelezwa na MORUWASA Manispaa ya Morogoro yenye thamani ya shilingi bilioni 18 ambayo itakuwa muarubaini wa kero ya maji Kata ya Kihonda, Mkundi na Lukobe fedha zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua miradi hiyo ya maji eneo la Kiegea Kihonda , RC Malima,  amewataka wananchi  kuhakikisha wanalinda  vyanzo vya maji ili miradi iwe endelevu pamoja na kuagiaza MORUWASA  kuhakikisha wanatoa matangazo ya kutosha kwa kushirikiana na Manispaa ya Morogoro ili wananchi waweze kulipia fedha na kuunganishiwa huduma ya maji  majumbani mwao.

"Rais wetu ametuheshimisha wana morogoro, tumepata miradi mingi ya maendeleo , kila sekta amegusa, sasa hivi mnaona maji tayari ,niombe sasa tulipe hizo fedha ili tuunganishiwe maji" Amesema RC Malima.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Rebeca Nsemwa, ameishukuru serikali kwa kuendelea kupeleka fedha nyingi za miradi ya maendeleo Wilaya ya Morogoro ikiwemo miradi ya maji iliyojengwa kwa viwango vya juu.

Nsemwa,  amesema mradi huo wa maji Manispaa ya Morogoro  unakwenda kumaliza kero ya maji i ya muda mrefu ambayo walikuwa wanaipata wananchi wa Kata ya Lukobe, Kihonda na Mkundi.

Naye, Mkurugenzi wa MORUWASA , Eng. Tamimu Katakweba, amesema wamejipanga vizuri kuhakikisha kila mwananchi ananufaika na huduma ya maji.

Katakweba,amesema kilichobakia ni wananchi kulipia shilingi 26,000/= kwa ajili ya kuunganishiwa huduma ya maji na wateja wa mwanzo 300 watakaolipia fedha hizo wataunganishiwa maji kwa siku 3 badla ya siku 7 kama ilivyo kawaidia ya kuunganishiwa huduma ya maji.

Pia, Katakweba ,amesema bado miradi mengine inakwenda kwa kasi hivyo maeneo mengine wananchi wakae mkao wa kula kwani Serikali inajitahidi kuhakikisha miradi inakamilika na kutoa huduma.

Miradi aliyoikagua katika ziara yake Januari 04/2024 ni mradi wa maji uliopo Kata ya Kihonda Mizani ambapo tayari wananchi wa Kiegea Kihonda wameshaanza kuonja matunda ya mradi huo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi katika kata hiyo,  wamemshukuru  Rais  Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwatua ndoo kichwani baada ya kumaliza kero ya maji ya muda mrefu.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.