FIKIRI AHIMIZA USHIRIKIANO MADIWANI NA WATAALAMAU ILI KUCHOCHEA KASI YA UKUAJI WA UCHUMI
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Morogoro Mjini, Fikiri Juma, amehimiza umoja na mshikamano baina ya madiwani , watumishi na wataalamu ili kuweza kuwatumikia vyema wananchi wa Manispaa ya Morogoro.
Ameyasema hayo kwenye Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani Manispaa ya Morogoro kwa robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2023/2024 uliofanyika Ukumbi wa Mikutano Ofisi Kuu ya Manispaa Januari 25/2024.
Fikiri, amesema kuwa Wananchi wanaimani na Viongozi wao hivyo ni jukumu la kuendelea kudumisha umoja, upendo na kufanya kazi kama timu ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi na kutimiza takwa la Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 inayotekelezwa chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha, amewataka Madiwani kutimiza wajibu wa kuwatumikia wananchi bila kuchoka ili kuleta maendeleo yao na hatimaye kuweza kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi.
Hata hivyo, Fikiri,ameendelea kupongeza juhudi za Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Rebeca Nsemwa, huku akisema Chama kupitia Ofisi ya CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, kitaendelea kumpa ushirikiano wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake.
Post a Comment