Header Ads

USAID KIJANA NAHODHA WAKABIDHI VIBUBU VYA KISASA VIKUNDI 172 VYA KUKOPESHANA MOROGORO

MRADI wa "USAID Kijana Nahodha ambao ni mradi maalumu kwa vijana unaofadhiliwa na watu wa Marekani kupitia shirika la maendeleo ya Kimataifa (USAID) uliopewa jina la " USAID Kijana Nahodha umeendeleea  kutoa fursa kwa vijana kwa kuwapatia Vibubu vya kisasa kwa Vikundi  172 vya Vijana Mkoa wa Morogoro kwa Halmashauri 3.

Vibubu hivyo vimegaiwa kwenye Ofisi ya Manispaa ya Morogoro Januari 21 kwa Halmashauri 3 zikiwa ni wanufaika ikiwemo Manispaa ya Morogoro wanufaika Kata 16, Moro DC Kata 16 na Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero 15.

Akizungumza katika uzinduzi wa ugawaji wa Vibubu hivyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, kuwepo kwa  mradi wa USAID KIJANA NAHODHA katika Manispaa  utasaidia vijana wengi kujikwamua katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Mhe. Kihanga, amesema vijana wa Morogoro kupitia mradi huo  wataweza kujitegemea vyanzo vya mapato endelevu, kushiriki katika maswala ya kiuchumi na kuwa na raia wenye tija wanaochangia kikamilifi ukuaji wa uchumi wa nchi.

Aidha, Mhe. Kihanga ,amesema ipo mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Manispaa ,hivyo Halmashauri zitaendelea kutoa ushirikiano katika kuwasaidia wananchi kiuchumi na hasa vijana.

Naye  Afisa  mradi wa USAID KIJANA NAHODHA Mkoa wa Morogoro, Toyi Dadi,amesema  utekelezaji wa mradi huo unaongozwa na T-MARC Tanzania kwa kushirikiana na mashirika ya Care International na  Tanzania Youth Coalition (TYC).

Toyi,amesema lengo la mradi huo ni kuwawezesha Vijana kiuchumi, afya pamoja na elimu ya uraia.

"Mradi huu utekelezaji wake ni wa miaka 4 na kwa sasa ni mwaka 2 wa robo ya pili ya utekelezaji, walengwa wa mradi huu ni vijana wenye umri kuanzia miaka 15-25 ambao wapo nje ya mfumo wa shule ambao hawasomi unaowakutanisha Vijana kujiwekea fedha kwa ajili ya kukopeshana na kujishughulisha na miradi ya kikundi na binafsi" Amesema Toyi.

Aidha, amesema Vibubu hivyo vitawasaidia katika kuhifadhi nyaraka za wana kikundi pamoja na  fedha za wanakikundi hadi pale watakapoanza kukopesha kisha fedha zilizobakia zitahifadhiwa benki kwa usalama zaidi.

Hata hivyo, Toyi,amesema katika mwaka 2024/2025 matarajio yao ni kuongeza idadi ya vikundi 100 na kufanya kuwa na jumla ya vikundi 272 wanavyo vihudumia.

Kwa upande wa Afisa Vijana Manispaa ya Morogoro , Jackline Mushi, amewataka Vijana hao watumie fursa za mradi huo kuvisajili vikundi vya ili viweze kuwa na sifa ya kupata mikopo ya Halmashauri.

Mradi wa USAID  KIJANA NAHODHA kwa Mkoa wa Morogoro umenza na  Halmshauri 3  ambazo ni Halmshauri ya Manispaaa ya Morogoro, Mvomero na Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro. 

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.