Header Ads

BMK MAFIGA YAPONGEZA MITAA ILIYOFANYA VIZURI ZIARA YA DIWANI.

 




BARAZA la Maendeleo la Kata ya Mafiga limeipongeza Mitaa iliyofanya vizuri katika kufanikisha uendeshaji wa mikutano mikuu ya mitaa kwa mujibu wa karenda katika robo mwaka ya 1 na 2 2023/2024 iliyokuwa ikiendeshwa na Diwani wa Kata hiyo, Mhe. Thomas Butabile.

Pongezi hizo zimetolewa januari 11/2024 kwenye kikao Cha Baraza la Maendeleo ya kata( BMK) kwa kuwapatia vyeti vya pongezi huku wakitambua thamani ya uongozi wao kwenye Mitaa.

Zawadi hizo zimeandaliwa na Diwani wa kata ya Mafiga Mh Thomas Butabile na Afisa mtendaji wa kata , Amina Said ambapo wamesema kuwa wamefanya hivyo kwa lengo la kuwatia Moyo na nguvu ili wazidi kufanya vizuri.

Mbali na hayo katika Baraza Hilo wamehudhuria watumishi wa Umma kutoka idara mbalimbali ikiwemo afya, sekretarieti ya Maadili,uhamiaji na Elimu.

Akizungumza katika Baraza hilo, Mhe. Butabile , amesisitiza suala la watoto kupata chakula shuleni na kutilia mkazo kwa wananchi ulipaji wa ada ya taka kwa wakati ili kufikia malengo waliyowekewa na Manispaa.

Nayw Afisa mtendaji wa kata ya Mafiga , Amina said, mefafanua kuwa sasa hivi ameunda Kamati ya Maadili hususani kuvaa nguo za heshima ofisini na kutumia lugha nzuri kwa kuwa wananchi wengi wamekuwa wakija ofisini kwake wamevaa nguo fupi hivyo ameomba Jambo hilo lifuatiliwe na kumteuwa Mtendaji wa Mtaa , Mwajuma Samgera kufuatilia mwenendo huo.

Mhe. Butabile alifanya ziara ya kurejesha yaliyofanywa na Serikali na yale ambayo Serikali inatarajia kuyafanya pamoja na kusikiliza na Kutatua kero za Wananchi katika Mitaa yote ya Kata ya Mafiga.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.