Header Ads

TFRA, TFC NA GST ZAINGIA MAKUBALIANO TASNIA YA MBOLEA




MAMLAKA ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) pamoja na Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) zimesaini Hati ya Makubaliano ya uzalishaji wa mbolea kwa kutumia rasilimali za ndani ili kutafuta namna ya kutekeleza mpango wa uzalishaji mbolea nchini kwa kutumia malighafi zinazopatikana hapa nchini.

Makubaliano hayo yameshuhudiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli pamoja na Wawakilishi wa Makatibu Wakuu kutoka Wizara za Madini, Nishati na Wizara ya Viwanda na Biashara wiki iliyopita Mkoani Dodoma.

Pia kikao hicho kimehudhuliwa na Maafisa kutoka taasisi mbalimbali za Serikali zikiwemo Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Akizungumza katika kikao hicho, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli amezihimiza taasisi hizo zilizoingia Makubaliano hayo kuanza kutekeleza yale yote yaliyopo ndani ya uwezo wa taasisi husika ili kikao kijacho wawasilishe taarifa ya yaliyotekelezwa.

Kukamilika kwa mpango huo kutaongeza upatikanaji wa mbolea na kutapunguza upungufu ambao umekuwa ukijitokeza mara kwa mara.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.