Header Ads

BARAZA LA WAZEE MANISPAA YA MOROGORO LAKUTANA KUJADILI TAARIFA YA KAZI 2023 NA MPANGO KAZI 2024













BARAZA la Wazee Manispaa ya Morogoro kupitia Mabaraza yake ya Kata wamekutana kwa lengo la kujadili  tathimini ya taarifa ya utendaji kazi mwaka 2023 pamoja na mpango kazi wa mwaka 2024.

Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Soko Kuu la Chifu Kingalu Morogoro Januari 19/2024 huku wakiwaalika wataalamu mbalimbali kutoka Ofisi za Serikali.

Akizungumza wakati wa Kufungua kikao hicho, Mwenyekiti wa Baraza hilo la Manispaa, Mzee Ally Rashidy  Zongo, amesema lengo ni kuona walipotoka na wanapoenda na kama kuna changamoto wazijadili kwa pamoja.

Mzee Zongo,ameyashukuru Mabaraza ya Kata kwa ushirikiano mkubwa wanaouonesha kwani mabaraza hayo asilimia kubwa yamekuwa yakifanya vizuri kila uchwao licha ya kuwepo kwa changamoto za hapa na pale.

"Tunasifika sana Morogoro Manispaa tumekuwa kinara wa kwanza kwa upande wa Mabaraza yanayofanya vizuri hii yote ni ushirikiano mkubwa mnaotupa Mabaraza ya Kata, endeleeni na ushirikiano wenu ,changamoto zipo lakini sisi kama Vongozi wa Juu tunaendelea na utatuzi" Amesema Mzee Zongo.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Morogoro, Mzee Samwel Mpeka, ameyataka Mabaraza ya Mkoa  kuzingatia malengo ya Baraza hayo ikiwemo  kujadili masuala mbalimbali yanayowahusu na kuweka mikakati ya kutatua changamoto zinazo wakabili ili Kuchochea maadili mema, uzalendo na ushiriki katika shughuli za ustawi na Maendeleo ya jamii Nchini.

Mratibu wa Wazee Manispaa ya Morogoro, Hamisa Kagambo,amewataka wazee kujenga tabia ya kutembeleana ili kujuliana hali pamoja na kudumisha upendo na mshikamano.

Afisa Afya kutoka Manispaa ya Morogoro, Martin Mzuwanda , amewataka Wazee kuzingatia lishe na kula vyakula vinavyotengeneza afya zao pamoja na kujenga tabia za kujua afya zao mara kwa mara.

Naye Katibu wa Baraza la Wazee Manispaa ya Morogoro, Dkt. Bakili Anga, amesema mpango uliopo ni kuhakikisha kwamba mabaraza yanakuwa na uwezo wa kujitegemea badala ya kutegemea wahisani.

' Niombe tusikate tamaa, najua zipo changamoto tunakumbana nazo lakini tushirikiane, tunao wadau wengie tuna watoto wenye uwezo tuwatumie hao katika kutatua changamoto zetu, wale ambao hawataki kwenda nasisi ambao waliingia kwenye uongozi wakidhani kuna fedha tutawaweka pembeni tubakie na wazee wenye moyo wa kujitolea na kuwatumkia wazee wenzao" Amesema Dkt. Anga. 

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.