Header Ads

KAMATI YA UTEKELEZAJI WAZAZI MKUNDI YAMTAKA MZAZI ALIYETELEKEZA WATOTO 6 KUJISALIMISHA.


KAMATI ya Utekelezaji Wazazi Kata ya Mkundi, imemtaka Mzazi aliyetelekeza watoto wake 6 kujisalimsha ifikapo tarehe 03/3/2023 ili kuwachukua watoto wake.

Kauli hiyo ameitoa Mwenyekiti wa Wazazi Kata ya Mkundi, Ndg. Daud Msuya, Machi 01/2023 akiongozana na Wajumbe wa   Kamati ya Utekelezaji Wazazi Kata ya Mkundi  pamoja na Polisi Kata katika ziara ya  kutembelea familia ya watoto 6  waliotelekezwa na Wazazi wao eneo la Kiegea B.

 Akizungumza katika ziara hiyo, Msuya, amesema alifanya mazungumzo na Baba wa watoto hao aliyepo Mkoa wa Tanga na kumtaka Baba mzazi wa watoto hao taehe 03/3/2023 arudi nyumbani mara moja kuwachukua watoto wake.

" Nimeongea na Mzazi wa watoto hawa, kwanza nimemtaka ifikapo tarehe 03/3/2023 arudi nyumbani kuwafuata watoto wake na yeye amekubali kurudi , lakini nimshukuru Polisi Kata wetu kwa ushirikiano wake wa kuwaomba Polisi barabarani kumsaidia kumrudisha mzazi huyo kwa kumpandisha katika basi bure  ili aje kuwachukua watoto wake" Amesema Msuya.

Katika hatua nyengine, Kamati hiyo imemuagiza Afisa Ustawi wa Jamii Kata ya Mkundi kuhakikisha watoto waliotelekezwa eneo la Kiegea B wanapatiwa mahala salama kwa kuishi .

Aidha, Msuya, amemshukuru Mwenezi wa Kata ya Mkundi, Ndg. Timoth Makasi kwa kuibua changamoto hiyo kwa kushirikiana vyema na Jumuiya ya wazazi ambao wana jukumu la moja kwa moja katika malezi ya watoto.

Hata hivyo, Msuya, ametoa pongezi kwa  Mwenyekiti wa Mtaa wa Kiegea B, Ndg. Mbwana Yohana pamoja na majirani wote lakini bila kumsahau ndg. Japheti Malambe kwa kutoa mahitaji ya kujikimu kwa watoto hao.

Mbali na hayo, amewashukuru Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji Wazazi Kata kwa kujitoa kwao na kutmiza majukumu yao kwa kutatua kero mbalimbali za wananchi pamoja na kutekeleza Ilani ya CCM.

Mwisho, amemshukuru na kumpongeza kwa dhati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukemea ukatili dhidi ya watoto na kuhakikisha vitendo vya ukatili vinatokomezwa.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.