KATA YA BOMA YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA KATIKA MAENEO YA UMMA NA SERIKALI.
KATA ya Boma Manispaa ya Morogoro imeadhimisha Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani kwa kufanya usafi.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Afisa Mtendaji Kata ya Boma, Prisca Mawala, amesema lengo la kufanya usafi ni kujikinga na magonjwa ya milipuko na yanayosababishwa na mazingira ya uchafu ukiwemo ugonjwa wa Kipundupindu,kuhara na Malaria.
“Leo sisi wanawake wa Kata ya Boma tumeadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kujitokeza kufanya usafi katika eneo letu la Ofisi ya Kata, eneo la Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya ghorofa, kwenye mitaro pamoja na eneo la Kituo cha Polisi Kata ambapo ujenzi unaendelea, lengo la usafi ni kuonyesha mfano na kuwahamasisha wakinamama wenzetu kufanya usafi kwa kujitolea wenyewe bila ya kushurutishwa ili kujiepusha na magonjwa nyemelezi na milipuko kama ugonjwa wa kipundupindu,kuhara hata na Malaria yanayotokana na wadudu wanaozaliana sehemu za mitaro isiyotembea na takataka zinazokaa kwa muda mrefu hivyo tumejitolea leo kufanya usafi ili tuwe mfano wa kuigwa lakini pia kumuunga mkono Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kampeni ya usafi " Amesema Mawala.
Mawala, amesema kuwa wanaendelea kuhamasisha wananchi kufanya usafi katika mazingira yanayowazunguka lakini pia ni wajibu kwa kila mtu kufanya usafi katika eneo lake pamoja na kutosahau siku ya juma la mwisho wa mwezi lililowekwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan la kufanya usafi katika mazingira yao.
Katika hatua nyengine, Mawala, amempongeza Diwani wa Kata ya Boma licha ya kutokuwepo lakini asilimia kubwa ya maandalizi ya shughuli hiyo Mhe. Diwani ametoa nguvu yake ya kufanikisha maadhimisho hayo.
Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Boma, Bi. Fitina Mhina,amesema kuwa amesema kuna baadhi ya wananchi hata wakinamama wamekuwa wagumu wa kushiriki kufanya usafi katika mazingira yao kutokana na hali jinsi ilivyo kuwa ngumu wanakuwa wanajikita kufanya biashara zao ili wajipatie kipato lakini wao kama wakinamama watawashauri wapange siku katika wiki wafanye usafi kwenye mazingira yao yanayowazunguka.
Bi. Fitina,amempongeza Afisa Mtendaji wa Kata ya Boma pamoja na watendaji wenzake kwa kuja na mpango wa kufanya usafi katika maadhimisho hayo.
Elimu iyotolewa leo katika maadhimisho hayo ni elimu ya kupinga vita dhidi ya ukatili wa kijinsia, ulinzi wa watoto pamoja na uundaji wa vikundi na mikopo ya wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu.
Post a Comment