DC NSEMWA AWATAKA WADAU WA SANAA KUCHANGAMKIA MKOPO WA ASIMILI 10 WA HALMSHAURI.
MKUU wa Wilaya ya Morogoro , Mhe. Rebeca Nsewa, amewataka waigizaji waliopo katika Tasnia ya Sanaa kujiimarisha katika kazi zao kupitia mkopo wa asilimia kumi unaotolewa na Halmashauri ya Manispaa.
Hayo ameyasema
katika uzinduzi wa mafunzo maalum ya uigizaji katika ukumbi wa soko la kingalu
Mjini Morogo yaliyofanyika Machi 03/2023.
“kwakua kuna
kiasi cha fedha kinachotengwa kwaajili
ya kusaidia vijana wenye nia ya dhati katika kuleta maendeleo, mnayosababu ya
kufuata utaratibu ili kupata fungu litakalosaidia kuleta ubora katika uzalishaji wa kazi zenu, nami
nitawasaidia kwa nafasi yangu ili kufanikisha hilo pale mtakaponihitaji’ Amesema
DC Nsemwa.
Hata hivyo DC
Nsemwa, amewataka wasanii kuzingatia
mafunzo ili kuonesha utofauti uliopo kati yao na wale ambao hawajapata mafunzo
hayo kwa kutengeneza kazi nzuri kitaalam zenye maudhui ya kuonesha matatizo
yanayoikabili Morogoro na njia za kuyatatua kama ukatili na unyanyasaji wa
kijinsia pamoja na athari zitokanazo na uharibifu wa Mazingira.
Aidha,
Katibu Mwenezi CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Maulidi Chambilila, amesema kwa
kuwa waigizaji hao wapo Jimbo la Morogoro Mjini ,hivyo Mbunge wa Jimbo hilo,
Mhe. Dkt. Abdulaziz Abood yupo pamoja na wasanii hao na atendelea kuwaunga mono
katika kufikia ndoto zao.
Chambilila,
amepongeza Uongozi wa Chama cha waigizaji Morogoro kwa kuandaa Mafunzo hayo
yenye lengo la kukuza Tasnia ya Sanaa na kuleta mabadiliko ya ubunifu wa kazi.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa waigizaji Mkoa wa Morogoro , Ramadhan Hamis Bugala , ametoa
shukrani za dhati kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro kupitia ofisi ya Utamaduni,Mkuu
wa wilaya ya Morogoro na Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini kuunga mkono zoezi
hili la utoaji mafunzo kwa hali na mali hadi kufanikiwa, ambapo waigizaji 50
wamepata mafunzo hayo na kutunukiwa vyeti maalum.
Mafunzo ya
uigizaji filamu yameratibiwa na chama cha waigizaji mkoa wa Morogoro
wakishirikiana na Bodi ya filam Tanzania na kutolewa na Muhadhiri wa chuo kikuu
Dodoma Dokta Gervas Kasiga kwa muda wa siku mbili tarehe 4 na 5 Machi 2023.
Post a Comment