Header Ads

WAZAZI WATAKIWA KUZINGATIA MAADILI YA WATOTO



KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Mwembesongo, David Meza , amewataka Wazazi na Walezi kusimamia na kuwaelekeza vijana wao kuzingatia suala la maadili hasa katika uvaaji wa mavazi yenye staha.

Meza , ameitoa kauli hiyo akiwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Kata ya Mwembesongo yaliyofanyika Macho 10/2023.

Aidha, amewataka Wazazi na Walezi  kuwajengea watoto misingi ya maadili, kuenenda vyema na utamaduni wa kitanzania.

“Kuna haja ya kurekebisha upya jamii tukianza na watoto katika suala zima la upendo na ushirikiano na wazazi tuache kuwa bize tuwape muda watoto, ili kama kuna viashiria vya ukatili wa kingono watueleze tujue mapema,”Amesema Meza.

Mtendaji wa Kata ya Mwembesongo, Sekela Benard , amesema kama wanawake wakisimama vyema katika majukumu yao anaamini vitendo vya ukatili vitaisha.

"Tusimamie maadili ya watoto wetu, Wazazi wengi tuko bize sana kutafuta fedha, hivyo hatushindi na watoto nyumbani na tukirudi tunakuta wamelala, tukiulizia tu wanaendeleaje basi na asubuhi tutatoka tena mapema, tupunguze ubize tujenge ukaribu na watoto wetu" Amesema Sekela.

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Mwembesongo, Neema Mang'ati, amesema ili vikundi kupata uhalali wa kukopeshwa lazima waunde vikundi vyenye kufuata shereia.

Pia,amesema ni marufuku vikundi kujichangisha kama havijasaliwa ili kuepusha migogoro ,huku akivitaka vikundi hivyo viundwe lakini viwe na tija ili viwe na sifa ya kukopesheka.

Kwa upande wa mtoa huduma ya afya  ngazi ya Jamii Kata ya Mwembesongo, Magreth Kanyinyi, amesema Kata ya Mwembesongo ni Kata iliyoongoza kwa utapiamlo lakini tangia kuanzishwa kwa mradi wa lishe endelevu kata hiyo imekuwa ya pili Manispaa kwa huduma nzuri ya lishe.

Mbali na shughuli hiyo , Viongozi walikata keki kwa ajili ya kuonesha upendo kwa wanawake   lakini Mtendaji wa Kata Sekela ,amegawa vikoi kwa wenyeviti wa Mitaa wanawake wa Kata hiyo ikiwa ni zawadi yake ya kutambua umuhimu wa  uwepo wa wanawake duniani.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.