Header Ads

MSUYA AWATAKA WAZAZI NA WALEZI KUWA KARIBU NA WATOTO WAO.


Wazazi na walezi wametakiwa kuwa karibu na watoto wao  kuhakikisha wanakuwa na maadili mazuri ili kupunguza matukio ya unyanyasaji na ukatili.

Kauli hiyo amesema ,Diwani  Kata ya Mbuyuni, Mhe. Samwel Msuya, katika Mkutano wa Baraza la Wazazi Kata ya Mbuyuni lililofanyika Machi 05/2023 kwenye Ukumbi wa Ofisi za Chama CCM Kata ya Mbuyuni.

Akizungumza katika Baraza hilo,  Msuya,  amesema wazazi wengi wameshindwa kufanya jukumu la malezi kwa kutokuwa karibu na watoto, wengi wao wakikimbizana na jukumu la kutafuta pesa jambo ambalo linawapa wakati mgumu walimu kuwa karibu na watoto kama wazazi

Hata hivyo, anaendelea kuishukuru Ofisi ya Ustawi  Kata ya Mbuyuni kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wazazi kuendelea kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia .

"Mbuyuni bado kwenye Malezi tupo nyuma sana, vitendo vingi vya ukatili vinafanyika lakini wazazi wanapuuzia na kumalizana, wazazi na walezi tujitahidi kukagua watoto wetu wanaporudi nyumbani , tujenge ukaribu na watoto , matukio haya ya ukatili yameshamiri, Viongozi wa Chama tushirikiane katika hili ili kuleta usawa katika Kata yetu na kutengeneza jamii nzuri, jambo hili nalivalia njuga na sitowavumilia watu wa namna hii katika Kata yangu" Amesema Msuya.

Aidha, Msuya, amesema Ilani ya CCM inaendelea kutekelezwa ambapo mpaka sasa wamejenga shule ya  Sekondari, utekelezaji wa Jengo la Utawala shule ya Sekondari Mbuyuni unaendelea, ujenzi wa matundu 20 ya Vyoo shule ya Sekondari Mbuyuni, Ujezni wa Ofisi mpya ya Kata pamoja na mpango wa ukarabati wa madarasa ya Shule ya Msingi Mbuyuni bila kusahau kuboresha barabara ili kurahishsa mawasiliano, 

Naye Katibu Elimu na Malezi  CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Ndg. Godwin Mlambiti, amesema Jumuiya ya Wazazi itakuwa bega kwa bega na Jamii katika kuhakikisha kwamba vitendo vya ukatili vinatokomezwa.

" Bahati nzuri Jumuiya yetu inafanya kazi moja kwa moja katika sehemu hii, hatutawavumlia watu wa namna hii, tumejipanga kama Kamati ya Utekelezaji kwa kuhsirikiana na Mwenyekiti wetu na ndio maana tumeanza ziara mashuleni kisha tutahamia Mitaani" Amesema Mlambiti.

Mlambiti ,pamoja na hayo ametoa salamu za Wilaya kwa Wajumbe wa Baraza huku akisema Mwenyekiti ana tambua kazi kubwa wanazozifanya Jumuiya ya Wazazi Kata ya Mbuyuni kwa kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi, Ofisi ya Kata na wananchi kwa ujumla.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Wazazi Kata ya Mbuyuni,Rehema Njayagha ,amesema Jumuiya imejipanga kuona jinsi ya kusonga mbele lakini pia amempongeza Diwani , Uongozi wa Chama kwa ushirikiano wanaoutoa kwao bila kusahau Uongozi wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya kwa kujitoa kwao na kujenga mahusiano mazuri na Viongozi wa Kata .

Katika Baraza hilo, jumla ya wananchama wapya 50 wamejiunga na Jumuiya ya Wazazi Mbuyuni na kupatiwa kadi zao mbele ya mgeni rasmi  Godwin Mlambiti.



No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.