Header Ads

KATA YA BIGWA YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUTEMBELEA MAKAO YA WATOTO YATIMA MGOLOLE


KATA ya Bigwa Manispaa ya Morogoro  imeadhimisha siku ya wanawake duniani katika kituo cha watoto yatima cha Mgolole Machi 07/2023.

Maadhimisho hayo yameambatana na kutoa misaada mbalimbali kwa watoto kama unga mchele, sabuni za kufulia, juice, sukari, madaftari, kalamu, mafuta ya kupaka na ya kupikia na vitu vingine vingi.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Bigwa,Helena Mgala, amewapongeza wadau waliojitoa kwa kuwathamini watoto yatima na wenye mazingira magumu kwa kuchagua kuadhimisha tukio hilo katika kituo hicho.

" wanawake ni jeshi kubwa na sisi tuliozaliwa na mwanamke tunamthamini sana mwanamke kwamba ndie mkombozi na Kila mwanaume aliefanikiwa basi kuna mwanamke nyuma yake” Amesema Mgala.

Naye Mwenyekiti wa UWT Kata ya Bigwa, Hadija Omary,  amewaomba sana wanawake wa Kata ya Bigwa  kuwasomesha watoto wao ili kuwaandaa kuwa viongozi wa baadae.

Kwa upande wa Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Bigwa, Mabula Masaba, ameushukuru uongozi wa kituo cha watoto Yatima cha Mgolole  kukubali kufanyia maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika kituo hicho.

Mabula,  amewaomba wakazi wa Kata ya Bigwa na Jamii kwa ujumla  kuwa mabalozi kwa watu wote kujitoa kwa moyo kukisaidia kituo hicho.

Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Bigwa, Mericiana Makanxa, amewataka wanawake kujitambua na kujielewa, kuamka na kuchakarika na kujihusisha na shughuli mbalimbali zitakazowaingizia kipato na sio kubweteka, kukaa kusubiri mwanaume awatimizie kila kitu.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.