MKUNDI WAADHIMISHA MIAKA 2 YA RAIS SAMIA KWA KUPANDA MITI NA KUOMBA MRADI WA MAJI KUKAMILIKA KUPUNGUZA GHARAMA ZA MAISHA KWA WANANCHI.
DIWANI Kata ya Mkundi, Mhe. Seif Chomoka akiwa na Diwani wa Viti Maalum, Mhe. Grace Mkumbae pamoja na chama Cha Mapinduzi CCM , wamewaongoza wananchi kuamua kuadhimisha sherehe za miaka 2 ya Uongozi wa Rais wa Awamu ya Sita, Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kupanda miti na kushiriki kwenye Kongamano wakiongozana na Wananchi katika mradi wa Tanki la Maji Mgulu wa ndege.
Akizungumza katika Kongamano hilo, Mhe. Chomoka, amesema zoezi hilo ni sehemu ya kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kampeni ya uhifadhi wa mazingira.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mkundi,Alex Mogwa, ameipongeza Jumuiya ya Wazazi CCM Kata ya Mkundi kwa kuja na mpango huo ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.
Diwani wa Viti Maalum, Mhe. Grace Mkumbae, amesema, kutokana na shughuli za kibinadamu ,miti mingi imekuwa ikikatwa na kupungua hivyo namna pekee ya kuirejesha ni kuhamasisha wananchi, taasisi mbalimbali za uhifadhi wa mazingira kushiriki zoezi hilo.
Naye Mwenyekiti wa Wazazi CCM Kata ya Mkundi ambaye ndio waandaji wa zoezi la upandaji wa Miti, Daud Msuya, amesema lengo la zoezi hilo ni kuhamasisha jamii kuendelea kutunza mazingira ili kuzuia athari hasi za mabadiliko ya tabia ya nchi zinazosabbishwa na kutokuwepo kwa miti ya kutosha.
Kongamano hilo la upandaji wa Miti liliratibiwa na Jumuiya ya Wazazi CCM Kata ya Mkundi kwa kushirikiana na Uongozi wa Kata kwa kushirikiana na Wananchi wa Kata ya Mkundi.
Mbali na upandaji wa Miti, Wananchi wa Mkundi walipaza sauti zao na Kumuomba Mhe. Rais kuwaangalia kwa jicho la kipekee la kuwezesha kukamilika kwa wakati kwa mradi huo kutoa huduma ya Maji na kupunguza gharama za maisha kwani ni muda mrefu tangia mradi uanze kujengwa huku wananchi wakiendelea kuteseka na suala zima la huduma ya Maji.
Wakati huohuo taarifa zilizotufikia ni kwamba wakandarasi washafika katika eneo la mradi huo wa Maji Mguru wa ndege.
Post a Comment