CRDB MOROGORO YAWASHAURI WANAWAKE KUFUNGUA AKAUNTI YA MALKIA
MENEJA Biashara wa Benki ya CRDB Tawi la Morogoro, Stephen Mapunda, amewashauri wanawake wa Morogoro kufungua akaunti ya Malkia kwa ajili ya kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima hali inayowafanya washindwe kufikia malengo yao kwa wakati.
Kauli hiyo ameitoa Machi 04/2023 katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kata ya Kihonda yaliyofanyika Ukumbi wa Magunila Kihonda.
Mapunda, amesema Malkia ni mpango mahususi kwa ajili ya
wanawake unaoelnga kuwapatia huduma mbalimbali za kibenki zitakazowasaidia
kuboresha uchumi na kuchochea maendeleo yao binafsi, familia na Jamii kwa
ujumla.
Aidha, amesema Malkia inalenga wanawake katika sekta mbalimbali
ikiwemo wajasiriamali , wafanyakazi, mama wa nyumbani na wastaafu.
Violele vile amesema Kupitia CRDB Malkia wanawake wanaweza
kupata huduma zifuatazo.
Akaunti ya Malkia
Ni akaunti maalum kwa ajili ya wanawake wenye lengo la
kuwekeza ili kutimiza ndoto zao za mafanikio iwe kwenye biashara, elimu au afya kwa kujiwekea akiba kidogo kidogo
kila mwezi.
Sifa za Akaunti ya Malkia
Kiwango cha chini cha kufungulia akaunti ni shilingi 5,000 ,
hakuna gharama za kila mwezi, riba inahesabiwa na kulipwa kila mwezi katika
amana yako, muda wa chini wa mpango wa
akiba ni miezi 12.
Faida,
Uwekaji akiba kwa malengo binafsi na familia, kiasi nafuu
cha kufungulia akaunti, inalipa riba nzuri kwa akiba uliyojiwekea, gharama
nafuu katika Uombaji wa mkopo, unaweza kupata mkopo mpaka asilimia90 ya akiba
uliyojiwekea, huduma za bure za mafunzo ya biashara ujasiriamalai na uwekezaji
pamoja na huduma za kipekee kutoka kwa Afisa Maalum wa Benki katika kila tawi.
Vigezo vya kujiunga,
Mwanamke mwenye umri wa kuanzia miaka 18 mpaka 70,
Kitambulisho chochote kinachotambulika Kitaifa (NIDA, hati ya kusafiria ,
kitambulisho cha kupigia kura au leseni ya udereva.
Mikopo ya Malkia
Malkia MSE
MSE Malkia inatoa fursa kwa wajasiriamali wadogo
waliosajiliwa na wasiosajiliwa kuweza
kukopa kwa jili ya kupanua mitaji ya biashara zao zikiwemo uchuuzi, viwanda
vidogovidogo , ufundi cherehani, watoa hudma , saluni na wengineo.
Sifa,
Inatoa fursa kwa waliosajiliwa na wasiosajiliwa , hutoa
mikopo ya mitaji, uwekezaji na pia manunuzi ya vifaa vya biashara, unaweza pata
mkopo mpaka shilingi milioni 50 , riba yake ni nafuu, muda wa kulipa mkopo
mpaka miezi 24, masharti nafuu , Uzoefu katika biashara usiopungua miezi 6 tu ,
hutoa fursa ya mafunzo ya biashara bila gharama yoyote.
Malkia SME
SME Malkia inatoa fursa kwa wajasiriamali wakati waliosajiliwa
kuweza kukopa kwa ajili ya kupanua mitaji ya biashara, kuongeza vifaa vya
biashara au uwekezaji.
Sifa
Biashara iliyosajiliwa, hutoa mikopo ya mitaji , uwekezaji
na pia manunuzi ya vifaa vya biashara, unaweza pata mkopo moaka shilingi
bilioni 3 , riba yake ni nafuu, Masharti nafuu katika dhamana, uzoefu katika
biashara usiopungua miezi 6 tu , hutoa fursa ya mafunzo ya kibiashara bila
gharama yoyote, muda wa kulipa mkopo mpaka miezi 60 kulingana na aina ya mkopo,
hakuna gharama ya uombaji wa mkopo na mafunzo ya uendeshaji wa biashara na
utunzaji fedha.
Malkia Kilimo (Agribusiness)
Malkia Kilimo inalenga wanawake wajasiriamali wadogo
waliosajiliwa na wasilosajiliwa ikihusisha wanaoongeza thamani ya mazao ya
Kilimo,ufugaji wa kuku, samaki au
wanyama , na kilimo cha matunda , mboga mboga n.k.
Sifa
Biashara iliyosajiliwa na isiyosajiliwa, hutoa mikopo ya
mitaji, uwekezaji na pia manunuzi ya vifaa vya kufanyia biashara, unaweza pata
mkopo mpaka shilingi bilioni 3, riba yake ni nafuu, masharti nafuu katika dhamana,
uzoefu katika biashara usiopungua miezi 6 tu, hutoa fursa ya mafunzo ya
kibiashara na usimamizi wa fedha bila gharama yoyote, muda wa kulipa mkopo
mpaka miezi 60 kulingana na aina ya mkopo na mtiririko katika biashara,hakuna
gharama ya uombaji wa mkopo na mafunzo ya uendeshaji na utunzaji fedha.
Sifa za kupata mkopo huu,
Post a Comment