Header Ads

ABOOD KAZINI: KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI JIMBO LA MOROGORO MJINI.

 


Leo tarehe 31.05.2022, Mh Abdulaziz M.Abood Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini amekutana na Wananchi mbalimbali  anaowatumikia Ofisini kwake,


Mh Mbunge amewasikiliza wananchi zaidi ya 80 waliofika ofisini na kufanikiwa kuwatatulia changamoto zao zikiwemo za Kuwalipia Ada na mahitaji mengine ya shule wanafunzi zaidi ya 10 wasioweza kumudu wanaojiunga na kidato cha tano uku akitumia zaidi ya tsh milioni mbili *(2,000,000)* kwa ajili ya jambo hilo, pia Mh Mbunge ametatua changamoto za kibinadamu kwa baadhi ya wananchi waliofika uku akishauri na kuwaelekeza wananchi wengine kwenda katika ngazi zinazofuata kwa utatuzi zaidi wa changamoto zao,


Sanjari na hilo Mh Mbunge amekabidhi hundi (cheque)ya tsh *milioni moja* kwa Boma mazimbu Jogging Club iliyolenga kuwasaidia kuinua mradi wao wa kununua matents(mahema) pamoja na viti kwa ajili ya kukodisha na kujiingizia kipato kama wanaclub wa michezo aina ya jogging hivyo kukuza uchumi wa kila mmoja, hii ikiwa ni kutimiza ahadi yake aliyoitoa alipokuwa Mgeni Rasmi kwenye jogging hiyo,


Sambamba na hilo Mh Mbunge amekabidhi hundi(cheque)ya tsh *milioni moja* kwa Jukwaa la Wanawake Mazimbu ambapo awali alikuwa Mgeni Rasmi na hii ikiwa ni kuwasaidia wanawake hao kiuchumi,


Baada ya Mh Mbunge kukutana na wananchi sasa anaendelea na Ratiba za vikao vya Bunge na shughuli nyingine za Kijimbo kama afanyavyo kila siku.


Imetolewa na,

Ofisi ya Mbunge

Morogoro Mjini

Slp 127

Morogoro


Mawasiliano ya ofisi

023 261 3892


Mawasiliano ya Mkononi

+255763552261

+255655056053

+255713719964


 *Karibuni sana*

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.