RC SHIGELA AWAPONGEZA WADAU WA MAZINGIRA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KUTUNZA MAZINGIRA.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela akipanda mche wa mti wakati wa Kongamano la wadau wa Mazingira lililofanyika Mei 20 mwaka huu Eneo la Magadu Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Mhe. Martine Shigela (wa pili kushoto) akiwa kwenye maandamano na wadau wengine wa mazingira kuelekea eneo la kupanda miti.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela akiongea na wadau wa mazingira siku ya Kongamano la Mazingira Mkoa wa Morogoro Mei 20 mwaka huu.
Mhe. Martine Shigela Mkuu wa Mkoa wa Morogoro (wa tano kulia, waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa mazingira Mkoa wa Morogoro .
Wakuu wa Wilaya akiwamo Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Gairo na Morogoro katika picha ya pamoja kwenye Kongamano la wadau wa Mazingira na kutoa michango yao namna ya kuhifadhi Mazingira. kutoka kushoto ni Mhe. Mathayo Maselle Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Mhe. Jabiri Omary Makame Mkuu wa Wilaya ya Gairo na Mhe. Albert Msando Mkuu wa Wilaya ya Morogoro.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Rosalia Rwegasira akipanda mti wakati wa Kongamano hilo.
Bi. Saada Shabibi (aliyeshika kipaza sauti) akitoa mchango wake wakati wa Kongamano la wadau wa Mazingira.
Wadau wa Mazingira Mkoa wa Morogoro wakiwa kwenye kongamano.
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Martine Shigela, amewapongeza wadau wa Mazingira Mkoa wa Morogoro wanaounga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha mazingira yanalindwa.
Ametoa pongezi hizo wakati aliposhiriki katika
Kongamano la wadau wa Mazingira Mkoa wa Morogoro lililofanyika Ukumbi wa Magadu
Mess Manispaa ya Morogoro.
RC Shigela, amesema
Serikali inatambua mchango wa taasisi zisizo za kiserikali ambazo kwa
namna moja ama nyingine zinashiriki kikamilifu katika suala zima la utunzaji wa
mazingira.
“ Leo tumefanya Kongamano kubwa la wadau, naamini changamoto zote tumeziwasilisha lakini kila taasisi ikifanya kazi kwa nafasi yake na kuzitatua changamoto hizo kwa kushirikiana na Serikali naamini kuwa kurudisha Uoto wa asili uliopotea katika Mkoa wetu wa Morogoro litawezekana kama tukiwa kitu kimoja, lakini niagize kila Taasisi sasa ziwe na utaratibu wa kuwa na vitalu vya miche ili tuwe na sehemu ya kupata miti kwa wingi na kaucha kutegemea sehemu moja kuchukua miche hiyo” Amesema RC Shigela.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando,
amepongeza jitihada za wadau wa mazingira na kuzitaka jamii kuutunza mazingira pamoja na misitu
iliyopo sambamba na kupanda miti kwani
unasaidia kunyonya hewa ya ukaa.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Jabiri Makame,
amesema upande wa Gairo kuna changamoto ya uharibifu wa mazingira hivyo kwa
kushirikiana na wadau wa mazingira atahakikisha anarudisha gairo ya Kijani huku
akianza na Kampeni ya Urithi wa Gairo aliyoizindua mwaka huu 2022.
Kwa upande wake Balozi wa Mazingira,Chage Alex, amepongeza
wadau wa mazingira kwa kuipokea vyema
Kampeni ya ‘Soma na Mti’ huku akisema kuwa Kampeni hiyo siyo tu ya
wanafunzi na wanachuo bali kila mtu anatakiwa ashiriki.
Chage,ambaye pia anasimamia kampeni ya Soma na Mti
ametoa rai kwa wazazi na walimu kwenye
shule na vyuo mbalimbali nchini kuwasimamia wanafunzi katika kushiriki upandaji
wa miti.
Chage, amesema kuwa, upandaji miti uende
sambamba na utunzaji ili kuhakikisha miti inakua,
hivyo kuifanya nchi yetu na Mkoa
wetu wa Morogoro kuendelea kuwa ya kijani hatua itakayosaidia kuhifadhi
mazingira.
Post a Comment