MANISPAA YA MOROGORO YAKABIDHI KOMPYUTA 30 NA PHOTOKOPI MASHINE 2 SHULE 3 ZA SEKONDARI NA VITUO VYA TRC.
MANISPAA ya Morogoro, imekabidhi jumla ya Kompyuta za mezani 30 kwa shule tatu 3 za Sekondari Mafiga, Kihonda na Kingolwira pamoja na Photokopi Mashine 2 kwa Vituo vya mafunzo vya TRC Kikundi na Kiwanja cha Ndege.
Tukio hilo la makabidhiano limefanyika leo Mei 02/2022 ambapo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Pili Kitwana amekabidhi huku ikishuhudiwa na Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Morogoro Chausiku masegenya , Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Sekondari Anna Lupiano pamoja na Afisa TEHAMA Manispaa Zenna Lutego.
Akikabidhi kompyuta hizo, Kitwana, ameishukuru Lanes kwa msaada huo huku akibainisha kuwa lengo la Manispaa ya Morogoro ni kuwa Manispaa ambayo ipo kiganjani ambao taarifa yoyote inaweza kupatikana muda wowote.
" Ninaamini kompyuta hizi zitawasaidia sana wanafunzi na walimu pia yapo mambo yatakayotatuliwa kupitia kompyuta hizi, ili sasa kuleta elimu bora, na kutengeneza wasomi wazuri ambao watachangia katika uchumi wa Taifa letu" Amesema Kitwana.
Kitwana, amesema vifaa hivyo vimetoka Wizara ya Elimu kupitia ufadhili wa Lanes.
Post a Comment