Header Ads

RAS MTUNGUJA ATOA WITO KWA WADAU WA LISHE KUONDOKANA NA LISHE DUNI















KATIBU  Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bi. Mariam Mtunguja, amewaasa wadau wa Lishe Mkoa wa Morogoro  kuunganisha nguvu zao na kuona njia bora ya kukwamua hali duni ya lishe kwa watoto walio chini ya miaka mitano baada ya takwimu kuonesha kuwa zaidi ya asilimia 43% ya Watoto wa umri huo hapa nchini kuwa na udumavu ukiwemo Mkoa wa Morogoro ambao unazalisha vyakula vya kila aina.

Hayo yamebainishwa Mei 23 Mwaka huu wakati wa Kikao cha ufunguzi wa Program Jumuishi ya Taifa ya Malezi na makuzi ya awali ya mtoto kupitia Hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala wa Mkoa huo Bi. Mariam Mtunguja, kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

Katibu Tawala huyo amesema pamoja na kuwa Mkoa wetu haupo ndani ya orodha ya mikoa kumi yenye idadi kubwa ya watoto waliodumaa inasikitisha kuwa bado Mkoa wa Morogoro unatajwa kuwa na hali ya lishe isiyoridhisha hali ywa kua Mkoa wetu kuwa na bahati ya kuzalisha vyakula vya aina mbalimbali.

“Na inasikitisha zaidi kwamba tunazalisha chakula kwa wnigi ikiwemo Mahindi, Mpunga, Matunda na Mbogamboga kila kitu tunacho lakini hali ya udumavu wa watoto wetu ni kubwa” amesema Bi. Mariam Mtunguja.


Aidha, Katibu Tawala huyo wa Mkoa, amebainisha changamoto zinazoweza kukabili maendeleo ya ukuaji wa watoto chini ya umri huo ambapo ili mzazi au mlezi aweze kubaini changamoto hizo, mzazi au mlezi huyo anapaswa kuwa karibu zaidi na mtoto kwa kipindi chote cha hatua za ukuaji wake.

“Asilimia 43% ya watoto wapo kwenye hatari ya kutofikia hatua timilifu na maendeleo ya ukuaji wao, kwa kusababisha na utapiamlo, kukosekana kwa uhakika wa chakula, miundombinu katika familia msongo wa mawazo, uhaba wa rasilimali pamoja na unyanyasaji wa watoto” amesema Bi. Mariam Mtunguja.

Katika hatua nyingine, Katibu Tawala huyo wa Mkoa kupitia hotuba hiyo ameweka wazi kuwa, maendeleo katika ukuaji wa mtoto ni matokeo ya Afua mbalimbali zinazohusisha wadau wa Sekta tofauti ambazo zina wajibika kutoa afua hizo kwa kuzingatia hali halisi ya huduma za malezi jumuishi kwa watoto wadogo kwa kutumia mifumo ya usimamizi na uratibu wa utoaji wa huduma hizo hapa nchini.

Kwa upande wakw Bi. Germana Mung’aho ambaye ni Afisa elimu wa Mkoa wa Morogoro amekemea baadhi ya walimu wanaowafanyia ukatili wanafunzi wa madarasa ya awali kwa kuwaadhibu inapotokea wamechelewa kufika shuleni na kutumia vyumba vyenye hali isiyoridhisha katika kuwafundisha, kwani kufanya hivyo kwa watoto hao ni kuchangia kuwadumaza kiakili na kimwili kwa kuwasababishia msongo wa mawazo na ulemavu kwa ujumla.

Akiwakilisha Wakurugenzi watendaji wa Mkoa huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Bi. Rehema Bwasi amebainisha kuwa kama watendaji watasimamia vema utekelezaji wa Progamu hiyo kwani malezi shirikishi na jumuishi katika makuzi ya watoto ni kitu cha muhimu katika kuwajengea uelewa wa kiakili na kimwili maishani mwao.


Naye, Afisa Programu wa Shirika binafsi la CHILDHOOD DEVELOPMENT ORGANISATION (CDO) ambalo ni watekelezaji wenza wa Programu hiyo Jumuishi Bw. Innocent Rusomyo ameweka wazi kwamba. Katika kutekeleza Programu hiyo wameanzisha na kutekeleza miradi kadhaa ya kuboresha elimu ya awali ya watoto katika kusaidia makuzi na malezi bora ya watoto ikiwemo mradi “MTOTO WETU TUNU YETU” ambao unatekelezwa katika Halmashauri tatu za Mlimba, Mvomero na Ifakara Mji.




No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.