Header Ads

RC SHIGELA AZINDUA CHANJO YA POLIO WATOTO CHINI YA MIAKA 5 MANISPAA YA MOROGORO.






MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Martine Shigela, amezindua mpango wa Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya Miaka 5 Manispaa ya Morogoro.

Uzinduzi huo, umefanyika Mei 18/2022 katika Kituo cha Afya cha Sabasaba kilichopo Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo, RC Shigela,amesema  takribani zaidi ya watoto 400,000 wenye  umri  chini ya miaka mitano wanatarajiwa  kufikiwa / kupatiwa chanjo ya kupooza  (Polio) katika Mkoa wa Morogoro.

"Kumekuwa na upotoshaji kuwa hii chanjo sio salama, Msiwe na shaka, Chanjo hii ya Polio ni salama kabisa na haina madhara yoyote na sio mara ya kwanza kuwa patia watoto wetu, hakikisheni watoto wanapewa chanjo hii, na wazazi toeni taarifa kwa wazazi wenzenu ili kuokoa taifa letu la kesho" Amesema RC Shigela.

RC Shigela, amesema kuwa mambukizi ya virusi vya Polio ni maambukizi yanayoathiri mfumo wa Neva na huweza kusababisha udhaifi wa misuli au Kupooza, ambayo ni kushindwa kusogeza misuli.

"kumbuka Matone mawili  ya chanjo ya Polio, Tanzania Bora Kesho" Okoa taifa la kesho kwa kupata chanjo" Ameongeza RC Shigela.

Naye, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kusirya Ukio, amesema kuwa Polio husambazwa kwa kugusana na mtu aliyeambukizwa,au kamasi na kinyesi chenye maambikizi.

Dkt. Kusirya, amesema Ugonjwa wa Polio huathiri zaidi Watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwasababu Kinga ya mwili yao iko chini. Dalili  za ugonjwa huo ni Homa,mafua, maumivu ya mwili, kichwa na shingo au ulemavu wa ghafla wa viungo vya mwili.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.