MUGAMBI AWASHAURI WATOTO WA KIKE KUVAA MAGAUNI 4 ILI KUTIMIZA NDOTO ZAO.
AFISA Maendeleo ya Jamii na mratibu wa dawati la maendeleo ya watoto Manispaa ya Morogoro, Joyce Mugambi, amewataka wanafunzi waz kike kuvaa magauni manne ili waweze kutimiza ndoto zao.
Kauli hiyo, ameitoa
mei 20/2022 katika hafla ya ugawaji wa taulo za mtoto wa kike zilizotolewa na Taasisi ya WEZESHA MABADILIKO kwa wanafunzi wa
sekondari wanaoishi katika mazingira magumu katika ukumbi wa mikutano wa
manispaa wa Kilakala Soko Kuu la Chifu Kingalu Morogoro.
Akizungumza mara
baada ya ugawaji wa taulo hizo, Mugambi, amesema kuwa wanafunzi wanatakiwa
kusoma kwa bidii ili wafikie malengo ikiwamo magauni manne ambayo ni sare za
shule, sherehe za kuagwa za kimasomo ya elimu ya Juu (graduation), Harusi pamoja na wanapoingia katika
majukumu ya kifamilia ya kuwa mama ambayo ndio hatua ya mwisho wa kufikia ndoto
zake.
Mugambi, amewasihi
wanafunzi wasiruke hayo magauni wakaharakia kuvaa magauni kwa kuvuka hatua za
uvaaji wa magauni hayo jambo ambalo litawapaelekea kutofikia malengo
waliojiwekea.
“ Leo mmeona jinsi
watu wanavyotambua umuhimu wenu, nanyi mnatakiwa msome kwa bidii haya magauni
mkayavae kwa hatua msiruke hata hatua moja, ukiruka hatua basi ujue unakwenda
kubaya, someni kwa bidii mfike chuo kikuu, mfanye sherehe zenu kama wasomi,
baaada ya hapo mtaingia katika hatua ya kuwa na familia yaani ndoa kwa kupata
mtu ambaye atakuwa chaguo lako na baada ya hapo utapata familia yako hapo
utakuwa umekamilisha safari ya mafanikio yako” Amesema Mugambi.
“Tungehitaji kuona wanafunzi wa kike katika Manispaa yetu ya
Morogoro wanajitambua, tusingehitaji
kuwa na wanafunzi wa kike wanaopata mimba wakakatisha masomo yao na ndoto zao,
natamani watoto wa kike wa Manispaa yetu ya Morogoro suala la elimu liwe Kipaumbele chao cha
kwanza” Ameongeza Mugambi.
Kwa upande wa
Mkuugenzi wa WEZESHA MABADILIKO, Dr. Lusako Mwakiluma,amewaomba walimu
kuwasaidia wanafunzi wa kike katika elimu ya kujitambua ili iwasaidie kuepukana
na vishawishi vinavyoweza kupekelekea mimba za utotoni.
Dr. Lusako, amesema si masuala yote ya yanayohusu maisha
yamewekwa katika mitaala, hivyo walimu wanapaswa kusimama katika nafasi zao
kama wazazi ili kile wanachotamani kuwafundisha watoto wao au ndugu zao kwa
lengo la kuwalinda na tabia zisizofaa, wakifanye pia kwa wanafunzi wao wa kike
ili wawasaidie wasiharibike
Naye Mkaguzi masaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, Inspekta Mwanaidi Lwena, ametoa wito kwa watoto wa kike kutokubali kutumiwa kama mitaji na wazazi wao kwa kukatishwa masomo na kuozeshwa mapema, ili kukabiliana na changamoto ya mimba za utotoni katika kufikia ndoto zao.
Inspekta Mwanaidi, amesema walimu wa kike wakiwasaidia na kuwa
marafiki kwa watoto wa kike ni rahisi watoto kuwaeleza matatizo yanayowakabili
na amewataka wanafunzi kuwa wazi kwa
walimu wao wa kike ili wasaidiwe.
Katika hatua nyingine wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwembesongo
Kidato cha 3, Neema Anthony,
wameiomba Serikali kuona namna ya
kuwashirikisha wazazi na walezi wao katika makongamano ambayo yanatumika kutoa
elimu ya masuala ya jinsia ili nao wawe na uelewa juu ya masuala hayo na kujua
namna ya kuwasaidia watoto wao.
Miongoni mwa shule za Sekondari ambazo wanafunzi wao wamegaiwa
taulo za Mtoto wa kike ni Mafiga, Uwanja wa Taifa, Nanenane, Tubuyu, SUA,
Kingo, Kihonda Maghorofani, Mwembesongo, Kayenzi pamoja na Uluguru.
Post a Comment