Header Ads

JUMUIYA YA AHMADIYYA MOROGORO YATOA MSAADA WA VYAKULA KWA ZAIDI YA KAYA 110 ZENYE UHITAJI.












JUMUIYA ya Kiislamu ya Ahmadiyya Morogoro imetoa msaada wa zaidi ya  Kaya 110 zenye uhitaji zilizopo  Kata ya Kihonda Maghorofani Manispaa ya Morogoro ikiwa ni chakula kwa ajili ya Mkono wa Eid Fitri ambapo utaratibu huo umekuwa ukifanyika kabla ya Sikukuu.


Hafla hiyo fupi ya ugawaji wa vyakula imefanyika leo Mei 09/2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ahmadya Kihonda Maghorofani.


Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo la ugawaji wa vyakula,DC Msando, ameomba mashirika na Taasisi zingine yakiwemo madhehebu ya dini kuelekeza misaada  mbalimbali kwa wananchi wenye uhitaji maalumu ili kutengeneza furaha na kudumisha umoja baina yao na wenye uhitaji .


DC Msando,ambaye ndiye mgeni rasmi  wa hafla hiyo fupi ya ugawaji wa chakula kwa wenye mahitaji akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Martine Shigela, amesema Ahmadiyya wamefanya jambo la uchamungu ambalo linatakiwa liigwe na Taasisi nyengine.


Naye Mkuu wa Chuo cha Jumuiya ya Ahmadiyya Morogoro, Sheikh Abid Mahmood Bhatti, amesema kuwa  msaada huo umetolewa kuunga mkono wito wa serikali inayohimiza mashirika,taasisi,na watu binafsi kutoa misaada kwa jamii yenye uhitaji.


Bhatti, amesema licha ya kuunga mkono Serikali i lakini pia kuweza kutoa zakatul Fitri kwa jamii ili kuweza kujumuika na jamii katika kusherehekea Sikuu ya Eid Fitr ambayo tayari imeshapita japo wamekuwa wakifanya kabla ya Sikukuu.


"Jumuiya ya Ahmadiyya ni moja ya sehemu inayojihusisha na utoaji wa misaada mbalimbali ikiwemo ya kiafya,kielimu na kijamii kwa kuwafikia watu wenye uhitaji, hivyo kutoa kwetu chakula kwa watu wenye uhitaji kwanza tumetekeleza misingi ya dini , kwani sisi tumekuwa tukifanya hivi kila ifikapo Siku ya Eid basi tumekuwa tukijumuika na ndugu zetu kuhakikisha kwamba tunakuwa nao pamoja katika kusheherekea sikukuu hii " Amesema Bhatti.


Miongoni wa vyakula hivyo vilivyo gharimi takribani Shilingi Milioni 2 na laki 5, ni pamoja na Mchele mfuko wenye  Kilo 5 na Unga wa Sembe Mfuko wa Kilo 10

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.