Header Ads

KUSAJIRI BIASHARA LAZIMA UWE NA ANWANI YA MAKAZI












NAIBU  waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea Mathew amesema hatua inayofuata sasa kuhusu anwani za makazi na Posti Kodi ni kwamba kila mwananchi anatakiwa kuwa na anwani za makazi na kwa wafanyabiashara hicho kitakuwa ni moja ya vigezo muhimu katika kutoa leseni zao za biashara.

“Wafanya biashara wote watakapokwenda kuomba leseni ya kufanya biashara, ni lazima atoa anwani yake ya makazi, asipokuwa na anwani ya makazi hataweza kusajiliwa  biashara yake” amesema  Naibu Waziri Kundo.

Waziri Kundo amesema hayo Mei 18/2022 ,wakati wa uzinduzi wa uwekaji wa vibao vya anwani za makazi katika Kata ya Kichangani Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro  alipofanya ziara ya siku moja.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.