Header Ads

KAMATI YA FEDHA MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO.


WAJUMBE wa Kamati ya fedha na Uongozi Manispaa ya Morogoro, wameridhishwa na utekelazaji wa miradi ya maendeleo, inayotekelezwa na  fedha za Umma Manispaa ya Morogoro.

Hayo wameyasema Mei 18/2022 katika ziara ya kamati hiyo baada ya kutembelea miradi ya maendeleo ikiwamo Kituo cha Afya Kata ya Lukobe, Jengo ambalo linahitaji kuendelezwa kuwa Zahanati Kata ya Mji Mkuu,  Shule mpya ya Sekondari Kata ya Mindu ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 72 pamoja na kukagua fremu zilizopo Soko Kuu la Chifu Kingalu kwa ajili ya kuangalia mwenendo wa ulipaji wa kodi kwa wafanyabiashara.

Aidha Wajumbe hao wamefurahishwa zaidi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo, huku wakiwataka wataalamu kuongeza nguvu ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Kaimu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Salma Mbandu,  amebainisha kuwa, Kamati hiyo ya Fedha, imeridhishwa na hali ya miradi yote iliyotembelewa na kuongeza kuwa hii ni kuonesha kazi nzuri inayofanywa na serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na mheshimiwa Rais mama Samia Suluhu Hassan.

"Miradi ni mizuri, imetekelezwa kwa viwango na ubora unaokubalika, imetekelezwa kwa kuzingatia Ilani ya Chama cha Mapinduzi pamoja na maenelekezo yanauotolewa na serikali, ikiwa na lengo la kuwahudumia wananchi  wote bila kujali itikadi zao, tunapongeza sana juhudi za Mheshimiwa Rais, Mama yetu Samia Suluhu Hassan" Amesema Mhe. Mbandu.

Naye Mjumbe  wa kamati hiyo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwembesongo, Mhe. Ally Kalungwana, amesema kuwa,  utekelezaji wa miradi hiyo, unapambanua juhudi za serikali  ya awamu ya sita kisekta, kwa kupanua wigo katika sekta ya elimu kwa kujenga vyumba vya madarasa  pamoja na kuongeza vituo vya afya ihususani Manispaa ya Morogoro ambapo kwa sasa kuna Vituo vya afya 2 vipo katika hatua za ujenzi.

Kuhusu, mwenendo wa kodi za walipanga katika fremu za Soko Kuu la Chifu Kingalu, Mhe. Zamoyoni Abdallah, amesema wadaiwa sugu wote wapewe barua za notes ili kuongezewa muda wa kulipa madeni na kama watashindwa basi maeneo hayo yatangazwe upya ili Soko liweze kujiendesha kupitia kodi za wafanyabiashara.



No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.