MEYA KIHANGA AWATAKA WANANCHI KUENDELEA KUPANDA MITI KURUDISHA UOTO WA ASILI.
MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amewataka wananchi wa Manispaa ya Morogoro kuendelea kupanda miti hususani katika maeneo yenye vyanzo vya maji ili kuondokana na tatizo la upungufu wa maji katika kipindi cha kiangazi.
Kauli hiyo,ameitoa Mei 21/2022 katika Kongamano la Wadau wa
Mazingira Mkoa wa Morogoro lililofanyika katika Ukumbi wa Magadu Mess Manispaa
ya Morogoro.
“Niwaombe sana wananchi wote wa Manispaa ya Morogoro,
tuendelee kupanda miti, tumeona Serikali imetaka kila Wilaya kupanda Miti
Milioni 1 la laki 5 sasa tuelekeze nguvu hiyo kupanda miti na kuitunza,
tukifanya hivi tutarudisha Uoto wa asili katika vyanzo vya maji ambavyo
vimeanza kupotea kutokana na baadhi ya Wananchi kuendesha shughuli zao
pembezoni mwa vyanzo vya maji ikiwamo Kilimo” Amesema Mhe. Kihanga.
Mhe. Kihanga, amewataka Watendaji wa Kata na Mitaa kwa
kushirikiana na Viongozi wa Mitaa kushirikiana kikamilifu kuhakikisha kwamba
wanakemea vikali wanaoharibu mazingira kwa kukata miti hovyo na kufanya
shughuli za kibinadamu pembezoni mwa vyanzo vya maji.
Post a Comment