ALLIANCE ONE YAKABIDHI MADAWATI NA MRADI WA KISIMA VYENYE THAMANI YA MILIONI 79 SHULE YA MSINGI KINGOLWIRA.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Albert Msando, akizindua mradi wa kisima cha maji shule ya Msingi Kingolwira uliofadhiliwa na Kampuni ya Tumbaku ya Alliance One.
Mradi wa kisima cha maji shule ya Msingi Kingolwira uliofadhiliwa na Kampuni ya Tumbaku ya Alliance One.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando,akiteta jambo na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kingolwira.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando, (wapili kutoka kulia) akipokea Madawati 300 yaliyofadhiliwa na Kampuni ya Tumbaku ya Alliance One.
Diwani wa Kata ya Kingolwira, Mhe. Madaraka Bidyanguze, (kushoto), akiwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro ambaye pia ni Afisa Elimu Msingi , Chausiku Masegenya (kushoto) wakipokea Madawati 300 yaliyofadhiliwa na Kampuni ya Tumbaku ya Alliance One.
Diwani wa Kata ya Kingolwira, Mhe. Madaraka Bidyanguze,akizungumza na kutoa pongezi kwa Kampuni ya Tumbaku ya Alliance One.
Mkurugenzi wa fedha kutoka Kampuni ya Tumbaku ya Alliance One , Festo Mwalonga, akimwakilisha Mkurugenzi wa Alliance One.
KAMPUNI ya Tumbaku ya Alliance One Tanzania (AOTTL) iliyopo Morogoro imemkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Albert Msando, Mradi wa kisima na Madawati 300 vyote vikiwa na thamani ya Milioni 79 kwa ajili ya Shule ya Msingi Kingolwira iliyo Manispaa ya Morogoro.
Tukio hilo la hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo limefanyika leo Mei 27/2022 katika Shule ya Msingi Kingolwira na kushuhudiwa na Viongozi mbalimbali kutoka Manispaa ya Morogoro pamoja na Viongozi wa Kata na Wazazi wa wanafunzi.
Msaada huo umekabidhiwa Mkurugenzi wa fedha , Festo Mwalonga, akimwakilisha Mkurugenzi wa Alliance One kwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro , Mhe. Albert Msando, katika halfa iliyofanyika Shuleni hapo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo, DC Msando, amesema kwa upande wa mradi wa kisima utasaidia kutatua kero za maji shuleni pamoja na msaada wa madawati ambao utasaidia wanafunzi kukaa katika mazingira rafiki darasani.
DC Msando, amewapongeza Alliance One kwa kuwa karibu na Jamii jambo ambalo linapaswa kuigwa na Taasisi nyengine katika kurudisha gawio kwa jamii kama sheria inavyosema.
"Leo ndugu zetu wametukimbilia kutusaidia , na niemapata taarifa sio mara yao ya kwanza , niwaombe sana waalimu endeleeni na moyo wa kufundisha kwani Serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki lakini kwa Wazazi wote hakikisheni mnafunga mkanda kwa kushirikiana na waalimu ili kuhakikisha wanafunzi na watoto wenu wanafikia malengo waliojiwekea , suala la malezi ya shule msiwaachie waalimu lazima mshirikiane kikamilifu kama mnataka matokeo chanya" Amesema DC Msando.
Mwisho, DC Msando, ameutaka Uongozi wa Shule hiyo kuhakikisha wanatunza vizuri misaada wanayopewa na wafadhili na kuiwekea miundombinu mizuri ili iweze kuwasaidia katika kizazi cha leo na kesho.
Naye Mkurugenzi wa fedha Kampuni ya Alliance, Festo Mwalonga, ameipongeza Serikali kwa kuweka Mazingira mazuri ya uwekezaji na ufanyaji wa biashara nchini , hatua ambayo imefanikisha Kampuni yao ya Alliance One kuweza kuona inatoa misaada kwa jamii ikiwemo kusaidiana na Serikali.
Naye Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro , Chausiku Masegenya, amewataka waalimu kuweka mikakati ya pamoja ili kuongeza viwango vya ufaulu.
Chausiku, ameishukuru Alliance One huku akiwataka kuto kata tamaa ya kuendelea kuwasaidia kwani bado shule hiyo imekuwa na changamoto nyingi zinazoikabili.
Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Kingolwira, Mh. Madaraka Bidyanguze, amesema Aliance One wamekuwa karibu nao kwa kila jambo na wamekuwa wepesi wa kusikiliza matatizo yao pale wanapokwenda kuomba msaad.
Mhe. Bidyanguze, ameomba wadau wengine kujitokeza kwa ajili ya kushirikiana na Serikali hususani katika kusaidia jamii ikiwamo huduma za elimu na masuala mengine mengine ya maendeleo.
Post a Comment