Header Ads

KONGAMANO LA SHIRIKISHO LA WAALIMU MKOA WA MOROGORO LA KUPONGEZA MAFANIKIO YA MWAKA MMOJA WA MHE. RAIS SAMIA LAFANA, DKT CASTICO AWAASA WALIMU KUFANYA KAZI KWA BIDII NA NIDHAMU,

KATIBU wa NEC Idara ya Organaizesheni na Mlezi wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Maudline Castico (kulia) akipokea zawadi iliyoandaliwa na Shirikisho la Waalimu Mkoa wa Morogoro kwa Rais Samia Suluhu Hassan.(kushoto) Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Comrade Fikiri Juma , (katikati) Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini , Comrade Chifu Sylivester Yared.

KATIBU wa NEC Idara ya Organaizesheni na Mlezi wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Maudline Castico (kulia), akimkabidhi cheti cha shukrani Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz Abood.

KATIBU wa NEC Idara ya Organaizesheni na Mlezi wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Maudline Castico, amezindua Kongamano  la Shirikisho la Waalimu Mkoa wa Morogoro la Kupongeza mafanikio ya mwaka mmoja  ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Kongamano  hilo limefanyika Mei 7/2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kilakala uliopo Soko Kuu la Chifu Kingalu Morogoro.

Akizungumza katika Kongamano hilo, Dkt. Castico, amewataka Waalimu  kufanya kazi kwa bidii, weledi na kuzingatia miiko na maadili ya kazi hiyo ili kufikia malengo ya Serikali katika kuogeza ufaulu wa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini.

Dkt. Castico, amesema kuwa  Serikali imewekeza fedha nyingi katika sekta ya elimu ili kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora, hivyo walimu hawanabudi kutekeleza majukumu yao kwa weledi na uadilifu ili kupata matokeo yanayoendana na thamani ya fedha inayowekezwa.

“Lengo la Serikali yetu inayoongozwa na Chama Cha CCM kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025  kwa upande wa taaluma ni kuhakikisha ufaulu wa wanafunzi unapanda kwa viwango vikubwa, na kuhakikisha ufaulu huo unaongezeka  ikiwa ni pamoja na kumudu stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu (kkk), Amesema Dkt. Castico.

Mwisho, amesema atahakikisha salamau zao anazifikisha kwa Mhe.  Rais Samia Suluhu , huku akiwataka Waalimu hao kuchapa kazi kwa bidii kwani Serikali ni sikivu na changamoto zao zitaendelea kutatuliwa kadri Serikali inavyoona inafaa ikiwamo malimbikizo ya madeni yao na upandishwaji wa madaraja  ili kuongeza Viwango vya ufaulu.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Dorothy Mwamsiku, amewapongeza Waalimu kwa kongamano hilo .

Mwamsiku, amesema hata katika ziara yake ya kukagua madarasa ya UVIKO-19 walimpa ushirikiano mkubwa na kufanya ziara yake kuwa ya mafanikio makubwa .

" Nimezunguka Mkoa mzima, walimu hawa wamefanya kazi kubwa, wameonesha uaminifu mkubwa kusimamia fedha za Serikali, Serikali inawapenda sana ndio maana imekuwa ikitafuta kila namna ya kuhakikisha stahiki zenu zinalipwa " Amesema Mwamsiku.

Katika hatua nyengine, Mwamsiku, amesema katika uchaguzi wa mwaka 2022, Chama kimejipanga vizuri katika kuleta viongozi wazuri na wachapa kazi ndani ya Chama.

Pia, amesema Chama kinapata ushirikiano mkubwa sana na Serikali hivyo kuwaomba Waalimu wakafanye kazi kwa bidii na pale kwenye changamoto Serikali ipo itazifanyia kazi.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Martine Shigela,  amewataka viongozi wa Serikali na Taasisi zake Mkoani humo hususani wanaohusika na kupandisha madaraja ya watumishi kufanya hivyo bila kusukumwa na bila kusubiri muda wa mwishoni uliotolewa na Serikali wa kupandisha madaraja hayo kwa watumishi wanaostahili.

" Tayari katika Mkoa wangu nimeshatoa maelekezo kwa Maafisa utumishi kuhakikisha kila mtumishi ambaye anastahili kupanda cheo apandishwe bila upendeleo wowote , na nina uhakika hilo nitalisimamia kikamilifu, niwatoe hofu Waalimu tembeeni kifua mbele Serikali yenu  chini ya Rais wetu mpendwa Mhe. Samia Suluhu Hassan inawapenda sana inawathamini na kuthamini kazi zenu pia" Amesema RC  Shigela.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Waalimu Mkoa wa Morogoro, Mwanafela Mkuu, amesema lengo la Kongamano hilo ni kuelezea mafanikio ya mwaka mmoja wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan kwenye Sekta mbalimbali ikiwamo Sekta ya Elimu ambapo walimu wameguswa kwa kiasi kikubwa na kuadhimia kufanya Kongamano hilo.

Mwanafela, amesema katika Kongamano hilo wameweza  kujadili na kutafakari mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye mwaka mmoja wa utendaji wake tangu aingie madarakani kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Machi 19, mwaka jana 2021.

‘Kongamano hili tumeliratibu vizuri ili kuonyesha mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi hiki cha mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wetu Kipenzi, mama Samia Suluhu Hassan, tumefarijika sana baada ya kilio chetu cha muda mrefu kufanyiwa kazi ikiwamo kupandishwa madaraja lakini kulipwa baadhi ya stahiki zetu ambazo waalimu wamekuwa wakizidai , tupo pamoja na Mama na tutafanya kazi kwa uzalendo mkubwa kuleta matokeo chanya katika Sekta ya elimu ” Amesema  ameongeza Mkurugenzi Omary.

Katika Kongamano hilo zaidi ya Waalimu 50 wameweza kupatiwa kadi zao za CCM na kuingizwa kwenye mfumo wa kadi mpya za Kijidigitali.

Mbali na Kadi, Shirikisho hilo walitoa  vyeti vya pongezi kwa baadhi ya Viongozi walikuwa bega kwa bega katika kufanikisha Kongamano hilo linafanyika na pia kumzawadia Mhe. Rais picha yenye sura yake kama ishara ya upendo  kwa waalimu hao lakini na picha yenye ubunifu iliyotolewa na Mkuu wa Morogoro baada ya kukabidhiwa na kijana mwenye mapenzi mema na Taifa hili.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.