KATIBU CCM MKOA MOROGORO AELEZA JINSI HAYATI MAGUFULI ALIVYOJITOA KWA WATANZANIA
KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Morogoro, Alexandria Katabi, amesema kuwa Hayati Magufuli katika uhai wake na nia njema kwa Taifa hili, alikuwa na nia ya dhati ya kukuza uchumi wa nchi na kuiletea Tanzania maendeleo.
Hayo ameyasema Machi 31/2021 katika ibada maalumu ya kumuombea Hayati ,John Pombe Magufuli, iliyoandaliwa na Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Morogoro iliyofanyika Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Jamhuri.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Katabi, amesema Hayati Magufuli, uzalendo wake lilikuwa ni jambo lisilo na shaka kabisa ambapo alikuwa mkali dhidi ya watumishi wake pindi akiona wanafanya mambo ndivyo sivyo na wala hakusita kufukuza kazi na kuweka wengine.
Katabi, amesema kuwa Hayati, amefariki huku nyuma akiacha miradi mingi mikubwa ambayo ikikamilika, itaiweka Tanzania katika ramani nyingine, Kuanzia ujenzi wa barabara, usambazaji wa umeme, miradi ya usafiri na alikuwa na kiu kubwa ya maendeleo katika huduma za kijamii.
" Tumeandaa zoezi hili kwa kuzingatia mema ya aliyekuwa Rais wetu Hayati Dkt. John Pombe Magufuli,kwa kumuombea ibada maalumu lakini ibada hii piatumeifanya kwa aliyeshika kijiti Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango tunawaombea waweze kuongoza Nchi Vizuri katika kipindi hiki kigumu cha majozi " Alexandria Katabi Katibu CCM Mkoa wa Morogoro.
Mwisho, amesema kuwa Hayati Magufli, alivutia wengi kwa msimamo wake usioyumba dhidi ya rushwa na ufisadi na matumizi mabaya ya mali za umma, daima aliwaza kuitoharisha nchi na vitendo hivyo ambavyo vilirudisha nyuma kasi ya maendeleo.
Post a Comment