Header Ads

MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM AGAWA FTARI NA DAKU MANISPAA UBUNGO NA KINONDONI.






Meya Jiji la Dar es salaam Mhe Omary Kumbilamoto kwa kushirikiana na Taasisi ya MIRAAJ TANZANIA pamoja na Taasisi ya ABDULLAH AID TANZANIA  ikiongozwa  na Mwenyekiti wao Ndugu Arif Surya (Arif Tanzania) waligawa ftari katika Manispaa ya Ubungo pamoja na Manispaa ya Kinondoni.


Zoezi hilo lilifanyika katika Manispaa mbili, Manispaa ya Ubungo katika Kata ya Ubungo pamoja na Manispaa ya Kinondoni katika Kata ya Mwananyamala ikishuhudiwa Meya wa Manispaa hizo tajwa hapo juu.


 Mhe. Kumbilamoto siku ya Apr 14 alikutana Mwenyekiti wa Taasisi ya ADULLAH AID TANZANIA pamoja na Taasisi ya MIRAAJ TANZANIA ndugu Arifu Surya na kukubaliana kugawa ftari kwa Kaya zote zenye huitaji katika Jiji la Dar es salaam.


Katika zoezi hilo la ugawaji wa ftari Mgeni Rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Mhe. Khamis Hamza Chilo, Aidha Mhe. Khamis amewapongeza waandaaji wote wa ftari hizo akiwemo Meya wa Jiji la Dar es salaam Mhe. Omary Kumbilamoto pamoja na Mwenyekiti wa Taasisi ya MIRAAJ TANZANIA na ABDULLAH AID TANZANIA ndugu Arifu Surya kwa kuzisaidia Kaya zenye huitaji hasa ukizingatia tupo katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.


Katika zoezi hilo jumla ya Kaya 600 ziliweza kunufaika na ftari hiyo pamoja na chakula cha daku, Kaya hizo ziliweza kupatiwa 

1.Mchele

2.Unga wa Ngano

3.Mafuta ya Kula

4.Sukari

5. Unga wa Sembe

6. Njungu Mawe.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.