Header Ads

MCHUNGAJI BUTABILE AWATAKA WATANZANIA KUWA WAMOJA.

Mchungaji ,Thomas Butabile, akitoa neno.


MCHUNGAJI wa kiroho , Thomas Butabile ambaye pia ni Mhe. Diwani wa Kata ya Mafiga, amewasihi watanzania kuendelea kuwa wamoja na kushirikiana kuijenga nchi yao, badala ya kubaguana.

Mchungaji Butabile , ametoa wito huo leo Aprili 03/2021kwenye Ukumbi Kilakala  wa Soko Kuu la Chifu Kingalu wakati wa ibada maalumu ya kumuombea Hayati Dkt. John Pombe Magufuli iliyoandaliwa Umoja wa Watendaji wa Kata Manispaa ya Morogoro.

Amesema Mwenyezi Mungu alimtoa mwanae wa pekee Yesu Kristo kuja kuikomboa dunia bila kuwabagua wanadamu, vivyo hivyo nasi binadamu tunapaswa kutobaguana, iwe kwa dini zetu, makabila yetu, mitazamo ya kisiasa na hata rangi zetu.

Aidha, Mchungaji Butabile, amewakumbusha watanzania kufanya kazi kama ambavyo vitabu vitakatifu vinasisitiza umuhimu wa kufanya kazi, na amebainisha kuwa Tanzania yenye neema inawezekana endapo kila mtu atazingatia kufanya kazi.

“Tukifanya kazi hatuhitaji hata misaada kutoka nje, nchi hii ina neema nyingi hata Hayati Magufuli alikuwa akiyatoa haya maneno jambo  ambalo tunapaswa kuishi nalo kwa vitendo'" Amesema Mchungaji Butabile.

Hata hivyo, Mchungaji Butabile,  amewaomba watanzania kuendelea kuliombea Taifa lao na pia kumuombea Hayati Magufuli aliyetangulia mbele za haki huku wakizidisha maombi kwa Rais wa sasa Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wa Tanzania ili waweze  kufanikiwa  kutekeleza jukumu kubwa na zito la kuiongoza nchi.

 Taifa.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.