Header Ads

TAPO YAKABIDHI MAJIKO 10 YA GESI KWA FAMILIA 10 ZENYE WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU MANISPAA YA MOROGORO.

zoezi la kukabidhiwa Majiko ya Gesi likifanyika.

Mratibu wa TAPO, Anthony Maskati.

TAASISI ya kusaidia watu wenye mazingira magumu Tanzania TAPO (Tanzania Ant-Povert Organization ) yakabidhi Majiko 10 ya Gesi Kampuni ya Oraxy kwa familia 10 zinazoishi katika mazingira  magumu Manispaa ya Morogoro.

Makabidhiano hayo yamefanyika leo Aprili 01/2021 Makao Makuu ya Ofisi hiyo yaliyopo Tushikamane Kata ya Kilakala Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mratibu wa TAPO, Anthony Maskati, amesema kuwa msaada huo wa Majiko 10 ya gesi ni kwa ajili ya kuwapatia faraja Watoto hao wanaoishi katika mazingira magumu waliowakilishwa na Wazazi wao.

"Moja ya sera ya Taasisi yetu ni kusaidia shughuli za kijamii ikiwemo kuunga mkono jitihada za Serikali za kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jamii ndio maana leo tumeona kuna umuhimu wa kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu Manispaa ya Morogoro wakiwakilishwa na familia zao" Amesema Maskati.

Maskati, amesema tangia kuanzishwa kwa shirika hilo, mpaka sasa zaidi ya watu 500 wameshapita katika mikono yao na kuwasaidia huku zaidi ya watu 100 tayari wameshakuwa na mafanikio yao na wanajitegemea wenyewe.

"Tumekuwa na mafanikio makubwa sana, lakini zaidi tunawashukuru sana Manispaa ya Morogoro kupitia kitengo cha Ustawi wa Jamii kwani tunashirikiana nao sana kadri tunavyotaka msaada kwao, lakini Serikali za Mitaa wamekuwa wakitupa ushiriako mkubwa sana wa kuwapata watoto, lakini Makao ya kulelea watoto kama vile Mgolole na Makao ya Masister wa Philipino wa Kisarawe Dar  Es Salaam kwani wao wamekuwa wakitusaidia sana na Kampuni ya Gesi ya Oraxy " Ameongeza Maskati.

Aidha ,amesema kuwa licha ya kuwasaida watoto wenye mazingira magumu katika misaada hiyo wamekuwa wakijihusisha na kuwalipia ada za shule watoto hao ili kuweza kutimiza ndoto zao.

Amesema licha ya mafanikio wanayoyapata lakini kumekuwa na changamoto ikiwamo baadhi ya vijana wanaosaidiwa katika masomo kutokufikia malengo kwani baadhi yao wamekuwa wakikatisha masomo kwa kuishia kidato cha tatu na kushindwa kuhitimu kabisa lakini kuwepo kwa wahitaji wengi katika shirika lao jambo ambalo ni changamoto lcha ya kusema bado wanaendelea kutoa huduma hizo na wanafikiria kutanua zaidi huduma kipindi watakapokuwa tayari kufanya hivyo.

Pia amesema kuwa,katika kuendesha Shirika hilo, kuna miradi mbalimbali wamekuwa wakiifanya ikiwemo mradi wa shamba lililopo Wilaya ya Mvomero Mbigili, mashine ya kusaga na kukoboa pamoja na ghala la kuhifadhia nafaka.

Ikumbukwe kwamba TAPO ilipata usajili mwaka 1999 lakini nyuma ya hapo ilikuwa tayari ishaanzishwa chini ya muasisi aliyeanzisha TUSHIKAMANE iliyopo Kilakala Manispaa ya Morogoro  ndugu Raija Saloneni.



No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.