DKT GWAJIMA AZINDUA WIKI YA CHANJO KITAIFA MOROGORO , AWATAKA WAZAZI KUWAPELEKA WATOTO VITUO VYA AFYA KUPATA CHANJO .
Waziri wa afya Maendeleo ya Jamii ,Jinsi Wazee na Watoto,Mhe. Doroth Gwajima,akizungumza na wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya uzinduzi wa wiki ya Chanjo Mkoani Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Loata Sanare, akizungumza na wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya wiki ya Chanjo Kitaifa Mkoa wa Morogoro.
Waziri wa afya Maendeleo ya Jamii ,Jinsi Wazee na Watoto,Mhe. Doroth Gwajima (katikati) akiwa amembeba mtoto mchanga kuashiria kwa uzinduzi wa chanjo Kitaifa. (kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, (kulia), Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Sheilla Lukuba.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga (kulia) akiwa katika uzinduzi wa wiki ya Chanjo Kitaifa.
Waziri wa afya Maendeleo ya Jamii ,Jinsi Wazee na Watoto,Mhe. Doroth Gwajima, akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa (kushoto), Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Sheilla Lukuba na Diwani wa Kata ya Chamwino Mhe. Aballah Meya, wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi waliojitokeza katika uzinduzi wa Chanjo.
Wazazi waliojitokeza katika chanjo
WAZIRI wa afya Maendeleo ya Jamii ,Jinsi Wazee na Watoto,Mhe.
Doroth Gwajima, amewataka Wazazi kuwapaeleka watoto wao katika vituo vya afya
ili waweze kupatiwa chanjo.
Kauli hiyo ameitoa leo Aprili 27/2021 wakati wa uzinduzi wa
Wiki ya Chanjo Kitaifa ambayo imefanyika Mkoa wa Morogoro katika Manispaa ya Morogoro
Kata ya Chamwino Viwanja vya Shule ya Msingi Chamwino B.
Aidha, Dkt.Gwajima, amesema kuwa watoto waliopata chanjo huwa
wamekingwa dhidi ya magonjwa hatari, ambayo kwa kawaida huweza kusababisha
ulemavu au kifo.
Amesema kuwa chanjo hutoa kinga dhidi ya magonjwa mengi
hatarishi huku akisema kuwa Mtoto ambaye
hajapata chanjo yuko katika hatari kubwa ya kupatwa na maradhi, ulemavu wa
kudumu au hata kupoteza maisha.
“Watoto wote wana haki ya kupata kinga hii, ”Chanjo ni njia bora zaidi kuzuia magonjwa ya
kuambukiza, hivyo Kila msichana na kila mvulana anapaswa kupata
chanjo kamili. Kinga utotoni ni muhimu sana” Amesema Dkt.Gwajina.
Katika hatua nyengine, amesema kuwa ni muhimu pia kwa kina
mama wajawazito kupata chanjo ya pepopunda ili kujikinga wao wenyewe na watoto
wao wanaozaliwa.
Pamoja na kwamba kuna maendeleo mazuri ya utoaji chanjo kwa
watoto katika miaka iliyopita,amesema ipo haja sasa kuanza kuvuka kutoka
asilimia 90 hadi kufikia asilimia 100 ya upatikanaji wa Chanjo ili kuendelea
kuokoa kizazi dhidi ya magonjwa.
Hata hivyo, amewataka wazazi na walezi wengine kuhakikisha
wanafahamu sababu za umuhimu wa chanjo,
ratiba ya chanjo inayotumika na mahali chanjo inakotolewa kwa watoto.
Dkt. Gwajima, ametoa wito kwa Wazazi wote au walezi wengine kuhakikisha kwamba wanazingatia ushauri wa mtaalamu wa afya kuhusu muda wa kukamilisha chanjo zinazohitajika.
Miongoni wa magonjwa mbalimbali yanayotolewa chanjo ni pamoja na surua na rubella,saratani ya shingo ya kizazi, kifua kikuu,kifaduro,kuharisha, nimonia, dondakoo,pepopunda,hoama ya ini, ulemavu wa ngozikama vile miguu au mikono au vyote kwa pamoja.
Katika Uzinduzi wa Chanjo Kitaifa, kauli mbiu ya mwaka huu 2021 inasema 'CHANJO HUTUWEKA PAMOJA, KAPATE CHANJO'.
Post a Comment