KUOKOTA CHUPA SI LAANA TENA, KWA SASA NI FURSA YA KIPATO.
Kaimu Afisa Mazingira Manispaa ya Morogoro, Dauson Jeremia, akiwa amebeba Plastiki Peving zinazozalishwa kwa kutumia chupa za plastiki ikiwa na lengo la kuondoa takataka za chupa za plastiki Mitaani.
Kaimu Afisa Mazingira Manispaa ya Morogoro, Dauson Jeremia (kushoto), akizungumza na mmoja wa wazalishaji wa Plastiki Peving, Jenipher Kaphipa.
Kaimu Afisa Mazingira Manispaa ya Morogoro, Dauson Jeremia,(kulia), akikagua uzalishaji wa wa Plastiki Peving (PV).
Zamani ilikuwa ni laana kuambiwa utaokota makopo, Siku hizi ni fursa ya biashara inayokuza kipato cha wote wanaoweza kufanya hivyo.
Kwa utamaduni wa siku nyingi ambao ulizoeleka
kabla ya teknolojia kuruhusu ufungaji wa bidhaa kwa namna tofauti zikiwamo
chupa za plastiki, watu wenye upungufu wa akili pekee ndiyo walionekana
majalalani wakiokota chupa na makopo.
Kutokana na maendeleo ya kiuchumi na ongezeko la uhaba wa ajira rasmi, hivi sasa kuna wanawake, vijana hata wazee, wanaookota chupa hizi kujipatia kipato.
Licha ya changamoto zilizopo, wanakabiliana nazo na kusonga mbele.
Bila kutambua ni lini mzigo wao utakuwa mkubwa
na wenye kilo nyingi ili waweze kupata pesa itakayotosha kukidhi mahitaji yao
muhimu mara baada ya kuuza.
Kutokana na mrundikano wa
takataka za Plstiki Mitaa, Shirika lisilo la Kiserikali la
Aqua-Alimenta-Tanzania (AA-TZ) lililopo Manispaa ya Morogoro ,chini ya
Mkurugenzi Yanga Mwangindo, wameweza kubuni mradi wa uzalishaji wa Plastiki Paving
(PV) kwa kutumia chupa za plastiki.
Akizungumza juu ya mradi huo
unaojulukana kwa jina la Solid Waste
Recycling ,Mkurugenzi wa Aqua-Alimenta-Tanzania (AA-TZ), Yanga Mwangindo , amesema
ubunifu huo umefanyika kutokana na mrundikano wa takataka za plastiki mitaani
ambazo zimekuwa zikichangia kwa kiasi kikubwa uharibu wa mazingira kutokana na
takataka hizo kutooza.
Mwangindo, amesema kuwa, ajira
hiyo ya ubunifu imekuwa ni ndoto kwao kuona ni kwa jinsi gani wanaweza kuzitoa
takataka za plastiki mtaani na kuzigeuza kuwa dili.
“Tumeanzisha ubunifu huu
baada ya kuona mtaani kumekuwa na tatizo kubwa la utunzaji wa takataka ngumu, na
hizi taka zimekuwa zikizalishwa kila siku jambo ambalo ni hatari kwa mazingira,
kwa kuona huu mpango unafanikiwa tumeona tushirikiane na Serikali yetu kupitia
Manispaa ya Morogoro ili kuweka nguvu za pamoja katika kusaidia Kampeni ya
pendezesha Mji lakini pia kuongeza ajira kwa vijana wetu kutokana na wimbi la
Vijana kukosa ajira “ Amesema Mwangindo .
Aidha, amesema kama ilivyo kwa biashara nyingine, changamoto hazikosekani ambapo amesema kuwa umakini unahitajika kwa wote wanaojihusisha na biashara hii hasa waokotaji.
Naye Kaimu Afisa Mazingira
Manispaa ya Morogoro, Dauson Jeremia, amepongeza jitihada za Shirika hilo kwa
ubunifu mzuri ambao una tija kwa usafi wa mazingira lakini umekuwa ukisaidia
kupata ajira kwa Vijana ambao wanajishughulisha na uokotaji wa taka lakini na
wale waliopo katika uzalishaji.
Jeremia, amesema nguvu iliyopo
kwa sasa ni kuhakikisha kuwa mradi huo unakuwa endelevu na unawafikia wananchi
wote wa Manispaa ya Morogoro katika kutunza mji safi na kupendezesha mazingira
.
Juma Nassoro ambaye ni
muokota machupa anasema amekuwa akitumia
zaidi ya muda mrefu kuzunguka mitaani,
kwenye daladala, baa, shule hata hospitali kuokota chupa hizo.
“Jua, mvua, vumbi, njaa, kudharauliwa na watu
vyote vinanisonga wakati natafuta chupa hizi kila mtaa ninaopita,” Amesema
Nassoro.
“Hatuna fedha ya kujikimu na
wajukuu zangu wanaelewa hilo hivyo hawana budi kuingia mtaani kuzitafuta tuweze
kununua chochote,” Ameongeza Nassoro.
Aqua –Alimenta-Tanzania
(AA-TZ) inajihusisha na Utengenezaji wa Plastiki Paving, urembo kupitia chupa
za vileo kwa ajili ya kupendezesha nyumba pamoja na mpango wa uzalishaji wa
Biogas ambapo kwa sasa wapo katika hatua za miwsho kukamilisha mradi huo.
Post a Comment