WANUFAIKA WA TASAF MANISPAA YA MOROGORO WATAKIWA KUTUMIA FEDHA WANAZOPEWA KWA MALENGO YALIYOKUSUDIWA.
Afisa Tawala Wilaya ya Morogoro, Hilary Sagara (kushoto) akiwa na timu ya Wataalamu kutoka Manispaa ya Morogoro leo Aprili 06/2021 wakati wa ziara ya kukagua walengwa wa TASAF Kata ya Mwembesongo Manispaa ya Morogoro.
WANUFAIKA wa TASAF Manispaa ya Morogoro wametakiwa kutumia kwamalengo yaliyokusudiwa fedha inayotolewa kupitia mpango wa kunusuru Kaya masikini unaotekelezwa na mfuko wa maendeleo ya Jamii nchini TASAF.
Rai hiyo imetolewa leo Aprili 06/2021 na Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro , Hilary Sagara, wakati wakizungumza na wanufaika wa mpango huo katika Kata ya Mwembesongo Manispaa ya Morogoro.
Sagara amefanya ziara fupi ya kukagua utaratibu mzima unaotumika waakati wa kugawa fedha hizo na kujionea namna ya wanufaika walivyotoa ushuhuda ni kwa jinsi gani walengwa hao wameweza kubadilisha maisha yao kupitia mpango huo wa kunusuru Kaya masikini.
Amesema kuwa Serikali kupitia TASAF ,imedhamiria kuondoa umasikini wa kipato unaowakabili wananchi wengi nchini na kwamba ili kuunga mkono jitihada za Serikali wananchi ambao ni wanufaika wa mpango huo wanapaswa kutumia fedha hizo kwa kilie kilichokusudiwa.
Amesema kuwa kumekuwa na taarifa kuwa baadhi ya wanufaika wa mpango wa kunusuru Kaya masikini wamekuwa wakitumia fedha hizo vibaya kinyume na malengo yaliyopo huku wengine wakitumia fedha hizo kuongeza wanawake kwa upande wa wanaume na wengine wakitumia kwa ajili ya uklevi jambo ambalo amelipigia marufuku na kuwataka wanaofanya hivyo kuacha mara moja .
Amesema kuwa mpango huo wenye lengo la kupunguza umasikini unatoa fedha hizo kwa ajili ya matumizi ya elimu, afya lakini cha ajabu wananchi wengi mara baada ya kupata fedha hizo wamekuwa wakibadilisha matumizi mazingira ambayo kila siku wamekuwa wakilalamika kuwa fedha hizo hazitoshi.
"Wananchi ni kweli kuwa pesa hazitoshi lakini kwa hiki kidogo mnachokipata ni vyema mkakitumia kwa malengo mazuri mliyojiwekea , haipendezi kuona mtu umepewa pesa ili umpeleke mtoto wako shuleni lakini hufanyi hivyo na badala yake unaenda kutumia kwa ajili ya ulevi, nawahakikishia kwamba Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro tutafanya ukaguzi wa mara kwa mara kuhusu fedha hizi" Amesema Sagara.
Amesema kushindwa kwa baadhi ya wanufaika kuzitumia fedha hizo kwa usahihi ndiko kunakopelekea wananchi kuendelea kuibebesha lawama kila siku Serikali kuwa imekuwa haifanyi kitu chochote cha maana katika kubadilisha pamoja na kuboresha maisha ya Watanzania.
Hata hivyo, amesisistiza kuwa kutoka sasa Kaya ambayo itabainika kutumia fedha wanazopewa kinyume na utaratibu basi upo uwezekano wa kuiondoa ili wapewe wale wenye shida ya pesa ambayo endapo ikitumika vizuri inaweza kubadilisha maisha ya wanufaika.
Post a Comment